Friday, 6 February 2009

Waziri Mkuu alikosea mara 2

Sakata la mauaji ya maalbino, waziri mkuu Mhe Kayanza Mizengo Peter Pinda alikosea.
1. Kutamka kuwa wauaji wa maalbino nao wauwawe. Matamshi yake yalikiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo yeye ameapa kuilinda.
2. Aliomba msamaha kwa masharti, kwa kutumia neno 'kama'.
'Kama' kuna mtu nimemkosea naomba msamaha. Alitakiwa aombe msamaha wa jumla kwani alikosea kwa asilimia 100.

No comments: