Monday 16 February 2009

Ushauri: Mliodhalilishwa mna haki kudai fidia

Pamoja na serikali kumvua madaraka aliyekuwa Mkuu wa Wilaya fulani (kule Kagera) kwa sababu za kuamrisha walimu wachapwe viboko na polisi, bado mimi naamini kuwa hiyo hatua haitoshi.

Ushauri wangu kwa walimu waliodhalilishwa na Mkuu wa Wilaya:

1. Wafungue kesi ya madai dhidi ya serikali kudai fidia ya fedha kutokana na udhalilishwaji hadharani uliofanywa na serikali. (walimu hao hawana hata kazi ya kutafuta ushahidi, kesi yao iko wazi). Hapa serikali ina kesi ya kujibu na inatakiwa kulipa fidia kwa kiwango abacho mahakama itaona kinafaa.
Pia asasi za kutetea haki za binadamu nchini ziwasaidie hao walimu ili kesi yao iandikishwe mahakamani -na walimu wapate haki yao. Hili litakuwa funzo kwa serikali na wawakilishi wake ili wakati wote wazingatie miiko, maadili ya kazi na kuheshimu katiba ya Jamhuri ya Muungano.

2. Walimu wahamishwe vituo vyao vya kazi kwenda vituo watakavyopenda wenyewe kwenda kufanyakazi.

No comments: