Friday, 6 February 2009

Danganya Toto!!

Makampuni ya kusambaza Umeme na Gesi UK yametangaza eti yanashusha bei ya bidhaa zao kuanzia mwezi ujao mwishoni ili kuwapunguzia mzigo watumiaji.
Hii ni danganya toto kwa vile wanajua wameshapata faida tayari. Imekuwa kawaida kwa haya makampuni kupandisha bei mwezi wa 9 au wa 10 (kipindi cha baridi kinapoanza) na kupunguza gharama za malipo mwezi wa 3 au wa 4 kwa vile msimu wa joto unakaribia kuanza.
Kwa hiyo hilo punguzo ni kiini macho tu. Kama kweli hayo makampuni yanajali basi yapunguze bei zake kuanzia Octoba na sio April!
Matumizi makubwa ya umeme na gesi huwa yako ktk kipindi cha msimu wa baridi (hasa Desemba hadi Machi) kwa hiyo wateja wa umeme wangeshukuru kupata punguzo kipindi hiki na sio kuwapunguzia bei pale ambapo hawahitaji kutumia umeme zaidi!
Haya watapunguza kwa sasa, lakini ikifika Septemba/Oktoba utawasikia -gharama za uendeshaji zimeongezeka na bei ya umeme na gesi imepanda kwa hiyo 'tunaongeza bei'!!!

No comments: