Thursday 25 June 2009

Ladies and Gents!

Niko Daa!
Ninafurahi sana kwa kila kitu; maisha ni mazuri, watu ni wacheshi n.k. Nchi imeendelea kwa kiwango cha kuridhisha na kama kuna dosari ni kidogo sana na zinarekebishika!
Kwa rafiki na ndugu zangu mlioko UK nawatakieni kila la kheri na mafanikio ktk shughuli zenu. 'Yapha' (hi nephew!/tom) na 'Mameki' (jerry) nanyi nawatakieni kila la heri na likizo njema. Be good boys eeeh! Salimia Mumy and Daddy!
Karibuni nyumbani TZ.

Wednesday 17 June 2009

God Help

.................
GOD Grant me the;
SERENITY to accept the things I can not change
COURAGE to change things I can, and
WISDOM to know the difference
.................

Favourite Books

New London Architecture 2
Kenneth Powell and Cathy Strongman
Merrell (London)
ISBN 13: 978-1-8589-4360-2
Price: £29.95

Frank Lloyd Wright 1867-1959
Building for Democracy
TASCHEN, Hong Kong 2004
ISBN: 978-3-8228-2757-4

Favourite Books

Building Quantities Explained
Ivor H Seeley
Paperback 432 pages
Publisher: Palgrave macmillan
ISBN: 9780333719725
Price: £30.99

Plumbing, 3rd Edition
R D Treloar
ISBN: 0-7506-6822-9
Price: £19.99

Building Regulations in Brief
Ray Tricker and Rozz Algar
ISBN: 0-7506-8058
Price: £19.99

Illustrated Building Pocket Book, 2nd Edition
Roxxana McDonald
ISBN: 0-7506-8015-6
Price: £19.99

The Architecture Student's Handbook of Professional Practice,
By American Institute of Architects
Price: £52.25

(source: www.waterstones.com)

'raffaeli'

raffaeli (wimbo wa kizazi kipya)

nilienda moja kwa moja kwa raffaeli,
nikamkuta nyumbani anasikiliza r kelly,
nikamuuliza raffaeli,
unayo cd ya makaveli?
akaniambia ana cd ya makaveli,
r kelly,
na maria carey.

Tuesday 9 June 2009

Thanks!

To you all 'silent readers' who spend your precious time going through this 'space'!

I am aware of your following and am humbled to realise that you value whatever I throw out here.

"Imagination. Creativity. Originality." -Quod Erat Demonstrandum

Bustani na maeneo ya kijani

Ktk nadharia ya mipango ya makazi (settlement planning) bustani na maeneo ya michezo zimegawanyika ktk madaraja kadhaa. Bustani sio kitu cha kukurupuka na kupachika tu popote utakapo!

1. Nyumba ya makazi (residential house) - kila nyumba inatakiwa itengewe eneo dogo la bustani. Kwa wenzetu wa UK karibu nyumba zote zina maeneo ya bustani kwa mbele au nyuma ya nyumba. Kwa sasa sina tarakimu za vipimo vya ukubwa wa bustani za kiwango hiki.

2. Kundi la nyumba (clusters) - kundi la nyumba 10 au zaidi linatakiwa kuwa na eneo lake kubwa kidogo la kuchezea watoto (play ground). Watoto au watu wa mtaa/mitaa jirani hukutana hapo kwa mapumziko ya muda mfupi ambapo pia watoto kucheza.

3. Bustani za kitongoji/kijiji (neighbourhood) - bustani hizi hukidhi mahitaji ya kitongoji au kijiji ambacho kina shule moja au mbili za msingi. bustani za kundi hili zina ukubwa zaidi ya zile za namba 1 na 2 hapo juu.

4. Bustani za 'wilaya' - hizi ni kwa ajili ya watu au eneo lenye vitongoji vingi (mathalani vitogoji zaidi ya 3) na lina maeneo ya maduka makubwa, ofisi za serikali/dola n.k. Bustani za daraja hili huwa ni kubwa zaidi ya zote hapo juu.

5. Maeneo yasiyowezekana kupangiliwa (cumbersome areas) - bustani za maeneo haya huwepo kutokana na kutokuwezekana kupangilia shughuli zozote, mfano za ujenzi wa nyumba za makazi ktk eneo husika na hivyo kutengwa kama eneo la kijani/bustani.

Kwa ujumla mji uliopangwa vizuri kwa kufuata kanuni za mipango miji huwa zina bustani za madaraja haya yote. Na inawezekana makundi tofauti ya bustani yakawa yanaungana ktk maeneo fulani (kutengeneza ukanda wa kijani) na hivyo kuwa mapito mazuri kwa waenda kwa miguu au baiskeli.

Panda Mti (mmea)

Lecturer wetu wa 'Landscape Architecture' (Liberatus Mrema) aliwahi kutuambia darasani vitu vitatu muhimu ktk maisha ya binadamu. Alitumia lugha ya kigeni kama ninavyomnukuu hapa, ila tafsiri ni yangu.
1. have a baby (mtoto)
2. plant a tree (panda mti)
3. write a book (andika kitabu)

'Bunge lafupishwa': Ni kama nilivyoshauri!

Naipongeza serikali na vyombo husika kwa kujali maslahi ya Taifa kwa uamuzi wao wa kufupisha kikao cha Bunge la Bajeti.

Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge, kikao kimeanza leo tarehe 09 hadi mwezi wa Julai mwishoni. Bajeti ya serikali itasomwa Bungeni tarehe 11.Juni.2009.

Itakumbukwa hivi karibuni nilitoa wito kuhusu kufupishwa kwa kikao hiki. Kwa hiyo uamuzi huu wa kulifupisha Bunge umenifurahisha mimi binafsi hasa kwa kuona kuwa serikali inasikiliza na kujali maoni ya wananchi! (ujiko!)

Ufuatao ni wito wangu nilioutoa tarehe 09/Mei/2009 kuhusu kikao cha Bunge la Bajeti 2009/10:

Saturday, 9 May 2009
Hali ngumu ya Uchumi: Bunge lifupishwe
Bunge la Jamhuri ya Muungano liko mbioni kukutana ktk marathoni ya vikao vya kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2009/10.

Kama wote tujuavyo, hiki ni kipindi kigumu sana kiuchumi duniani kote. Ni vizuri viongozi wetu na wawakilishi wetu wakazingatia hali tuliyonayo na kuchukua hatua za kusaidia kupunguza makali ya uchumi.

Mojawapo ya hatua za kuchukua ambazo ziko ndani ya uwezo wetu ni kufupisha urefu wa vikao vya Bunge. Kwa kawaida vikao vya bajeti huchukua miezi miwili (Juni hadi Agosti kila mwaka).

Napendekeza kwa waandaaji wa ratiba za
1. hotuba za mawaziri kuwasilisha bajeti na
2. muda wa waheshimiwa wabunge kujadili bajeti hizo,
zifupishwe kwa asilimia 10 au zaidi.

Hotuba kuu ya waziri wa fedha na wa mipango kuhusu hali ya uchumi wa nchi ndizo zipewe muda wa kawaida, lakini hotuba zote za wizara zinazofuata zifupishwe kama nilivyopendekeza kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

Haitakuwa uamuzi wa busara kutumia gharama kubwa kuendesha vikao wakati huduma muhimu kwa wananchi zinayumba kwa kukosa fedha za kuziendesha. Kama wananchi wanaambiwa wafunge mikanda kila siku, inakuwaje wakubwa waendelee kulegeza ya kwao?

Kila mtanzania ana wajibu wa kubana matumizi ktk nafasi yake aliyoko, na nyie wawakilishi wetu fanyeni vivyo hivyo!


(source: mosonga blog; Saturday, 9 May 2009)

'Gordon toa makaratasi'

Jana Waziri Mkuu wa UK Gordon Brown alifanya kikao na wabunge wa kutoka chama chake cha Labour ktk harakati za kutuliza vumbi la misukosuko ndani ya chama hasa baada ya Labour kufanya vibaya ktk chaguzi mbili (za serikali za mitaa na wabunge wa bunge la ulaya). Ktk chaguzi hizo Labour ilifanya vibaya sana na hata kujikuta ikishika nafasi ya tatu chini ya 'makonsevativu' na chama kidogo cha 'ukip'.
Pia matatizo ndani ya Labour yalisababishwa na wabunge kudai malipo ya masurufu (expenses) hata ambayo hawakustahili kulipiwa na serikali! Ktk sakata hili baadhi ya mawaziri na manaibu kadhaa ilibidi waachie ngazi na wabunge kadhaa nao kutangaza kuachia ngazi ktk uchaguzi ujao (hawatagombea tena)!

Ktk kikao cha jana jioni, wabunge walimwambia WM Brown 'asafishe nyumba' la sivyo ataachishwa kazi!

Miongoni mwa masharti aliyopewa ili waendelee kumuunga mkono ni kufuta sera yake ya kubinafsisha (partly privatisation) shirika la posta na Royal Mail. Wabunge wengi hawaungi mkono ubinafsishaji wa Royal Mail. Pia WM ameambiwa alinde ajira za wafanyakazi ambao inaelekea wengi wao wako ktk hatihati ya kupoteza ajira zao ktk makampuni na mashirika kadhaa. Kuna baadhi ya sera mpya za WM Brown ambazo hazikuwafurahisha wabunge na wananchi kwa ujumla ambao ndio wapiga kura. Kwa mfano kuondoa kiwango cha kodi cha watu wa kipato cha chini cha asilimia 10 na kukifanya kuwa asilimia 20 kwa wote (flat rate) - uamuzi huu umewaumiza watu wengi sana wa kipato cha kawaida. Hata matajiri nao hawakufurahishwa na uamuzi wa serikali wa kuongeza kiwango cha kodi kutoka asilimia 40 hadi 50.

Suala la uhamiaji nalo bado linaisumbuia serikali na limechangia pia kushindwa vibaya kwa serikali ktk uchaguzi. Hata hivyo baadhi ya wabunge wamemtaka WM Brown awahalalishe wanaoishi na kufanya kazi UK bila vibali ili waweze kuwa raia kamili na kushiriki kikamilifu ktk kuijenga nchi yao. Wabunge hao wamekasirishwa na uamuzi wa serikali kuendelea kutowatambua watu wanaoishi nchini bila vibali. Mbunge mmoja alisisitiza mbele ya mtangazaji wa tv nje ya ukumbi wa bunge kwa kusema 'hawa watu wapo nchini, na pia wanafanya kazi kichini chini, ni kwanini wasipewe vibali (makaratasi)?

Mpende mwenzako

"Mtu hawezi kujipenda yeye kwanza kabla hajampenda mwenzake, hivyo mioyoni mwetu yatupasa kujenga tabia ya kuwapenda wenzetu kabla ya kujipenda sisi."
-Padri Josephat Mosha wa Kanisa Katoliki Parokia ya Chang’ombe mkoani Dar es Salaam

chanzo: habari leo.co.tz 08.Juni.2009

Monday 8 June 2009

Favourite Books

A. Architecture:

Understanding Housing Defects,
2nd Edition
Duncan Marshall, Derek Worthing and Roger Heath
ISBN 0-7282-0417-7
Price: £29.00

Building Construction Handbook,
7th Edition
Roy Chudley and Roger Greeno
ISBN 978-0-7506-8622-8
Price: £23.99


B. Research:

Research Methodolgy: A step by step Guide for Beginners
Ranjit Kumar
1990
Pages; 352
Price; £24.99

Research Methodolgy: Tools, Techinique
Gopal Lal Jain
Pages; 304
30/03/1998
Price: £30.00 (?)

PACD

Pledge. Aspiration. Commitment. Determination

Saturday 6 June 2009

D-Day Landings, Normandy

65th anniversary today! Ceremony attended by PM Gordon Brown (UK), Prince of Wales (Prince Charles), President Barrack Obama (US) and their host President Sarkozy of France.

Jicho la 3: "Kimbelembele"

Na tuwe wakweli: Hakuna jambo kubwa lililofanyika katika historia ya dunia bila kusimamiwa na watu ambao wangeweza kusemwa kwamba wana ‘kimbelembele’.

Hatari ya kujitokeza na kuchukua nafasi ya mbele katika jambo lo lote ina zahma zake, kama ambavyo historia inatufunza.

Yesu Kristo asingewambwa msalabani kama angetulia Nazareti akatengeneza vitanda vya samadari akawauzia wakoloni wa Kirumi.

Patrice Lumumba asingechinjwa na kuyeyushwa katika mapipa ya tindikali kama angekubali ubeberu ufanye unavyotaka nchini Kongo, wala Nelson Mandela asingefungwa kwa miongo mitatu kama angekubali kwamba ni ada ya mtu mweusi kumtumikia mtu mweupe.

Wote hawa walikuwa ni watu wa ‘kimbelembele’ cha aina fulani, ‘kimbelembele’ kilichowasukuma na kuwaweka mbele ya wenzao, wakati mwingine bila hata kujua kwamba walikuwa wamesimama mbele, wanaonekana, na kwa hiyo ni mabango ya shabaha.

Issa Shivji angeweza akabakia katika taaluma ya uwakili na akatengeneza ‘vijisenti’ vya kutosha na akaendesha gari linalofanana na la profesa wa kisasa (achana na magari ya akina Calculus). Lakini amejitokeza, akasimama mbele katika masuala kadhaa. Ana kimbelembele.

Masoud Kipanya angeweza akachora picha za ndege wanafurahi angani, au jua linakuchwa magharibi mwa Kigoma na zikampa utajiri mkubwa kutoka kwa watalii na Wazungu waliopotea njia. Asingekuwa kiongozi bali angekuwa mchoraji tajiri, kwa sababu angekuwa amekosa kimbelembele.

Lakini Kipanya ni kiongozi kwa sababu amesukumwa na kimbelembele kitakatifu kutumia sanaa yake kujenga demokrasia na jamii iliyo bora nchini mwake. Ni kiongozi.

Filbert Bayi (Christchurch, 1974) angeweza akabaki ndani ya kundi kubwa la wakimbiaji, asichukue ‘risk’ ya kujitanguliza na kujifanya shabaha, na akamwachia John Walker ashinde mbio zile, rekodi ya dunia isingevunjwa siku hiyo.

Alichofanya Bayi ni kwamba mara aliposikia mlio wa bunduki, aliruka na kwenda mbele ya kila mtu, na akabakia mbele hadi mwisho wa mbio hizo. Kimbelembele chake kikaleta sifa ambayo haijawahi kuletwa na mtu mwingine nchini Tanzania.

Naam, kiongozi hana budi kuwa na kimbelembele!



source: raia mwema (rai ya jenerali)

Msamiati

Maneno mapya ambayo yanatumika sana ktk lugha yetu ya Taifa.

Asasi - organisation
Mchakato - process
Mdau (mshika dau) - stake holder
Mlengo (wa kulia/kushoto) - (right/left) wing
Mstakabali - future
Mtandao - network
Ngono - sex
Sera - policy
Ubia - partnership/joint venture
Utandawazi - globalization
Weledi - professionalism

Friday 5 June 2009

Jamii na maisha

Mvuto kwa vijana wa jinsia nyingine
Kuwa na hamu ya ngono ni sehemu ya ujinsia. Kufanya ngono ni namna moja ya kuonyesha ujinsia , lakini ia unaweza kuonyesha ujinsia huu kwa kuongea, kushikana mikono, kupigana busu, kushikanashikana na kupapasana.

Mara nyingi madhumuni ya kufanya ngono ni kutaka kuzaa mtoto. Sababu nyingine za kufanya ngono ni kwa kujifurahisha, kuonyesha mapenzi na kuimarisha uhusiano wa kimapenzi. Jambo la msingi ni kuwa hapo utakapoamua wakati umefika wa kujihusisha na ngono umefika zingatia hiyo ngono iwe salama na kuwa wote yaani wewe na mwenzi wako mifurahie hiyo ngono.

Zamani au hata mila na desturi na desturi zetu zimetufanya tufikiri kwamba mwanamke pekee yake ndiye mwenye jukumu la kumfurahisha mume kwenye ngono bila mume kujali kama mpenzi wake naye ametoshelezwa.

Siku hizi angalau mambo yameeanza kubadilika na wanaume wengi wanatambua umuhimu wa kujali kumtosheleza mwenzi wake wakati wa kujamiiana. Tendo la ngono linakuwa nzuri pale wote wahusika watakapokuwa wamefanya kwa hiari, wametoshelezana na ngono hiyo ilikuwa salama ( hakuna mimba kama haikutakiwa, wala magonjwa ya zinaa au maambukizo ya UKIMWI)


chanzo: tovuti ya cheza salama (tanzania)

Character in hard times essential

'great character is forged through hardships'
-daily news, november 23, 2006

Mwelekeo wa Bajeti ya 2009/10 TZ

Bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha wa 2009/10 inatarajia kupanda kutoka Sh. trilioni 7.2 za mwaka huu hadi Sh. trilioni 9.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 32, ambayo imeainisha maeneo sita ya kipaumbele.

Akifafanua vipaumbele vya bajeti hiyo ambayo inatarajiwa kusomwa Alhamisi ijayo mjini Dodoma, Mkulo alisema:

-kipaumbele cha kwanza ni elimu ambayo imeongezewa fedha kwa asilimia 22 kutoka Sh. trilioni 1.4 ya mwaka 2008/09 hadi Sh. trilioni 1.7 mwaka ujao wa fedha. Lengo la kutenga kiasi hicho cha fedha ni kuimarisha ukaguzi wa elimu kwa ngazi zote nchi nzima.

-kipaumbele cha pili ni miundombinu ambayo bajeti yake imeongezeka kwa asilimia 12.7 ikilinganishwa na mwaka 2008/09. Katika mwaka wa fedha wa 2009/10, Wizara ya Miundombinu imetengewa Sh. trilioni 1.0 ikilinganishwa na bajeti inayomalizika ya Sh. bilioni 973.3. Serikali inatarajia kuboresha barabara, madaraja, bandari, viwanja vya ndege, kuimarisha mashirika ya reli (TAZARA na TRL) na Shirika la Ndege (ATCL).

-kipaumbele cha tatu ni afya ambayo imetengewa Sh. bilioni 963.0 kutoka Sh.bilioni 910.8 mwaka 2008/09. Kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, bajeti itajikita katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM), kuimarisha ubora na upatikanaji wa huduma za uzazi na mtoto na kuimarisha rasilimali watu katika ngazi zote.

-kipaumbele cha nne ni kilimo ambacho kimeongezewa bajeti kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo bajeti ya wizara hiyo imepanda kutoka Sh. bilioni 513 mwaka unaomalizika hadi Sh. bilioni 666.9 mwaka ujao. Fungu kubwa katika sekta hii linaenda katika kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za kutosha kwa wakulima na wafugaji. Waziri Mkulo alisema katika kutekeleza kaulimbiu ya 'Kilimo Kwanza', serikali itaweka msukumo katika uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na mifugo, viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa kwa kushirikiana na sekta binafsi.

-kipaumbele cha tano ni Wizara ya Maji ambayo imetengewa Sh. bilioni 347.3 mwaka huu kutoka Sh. bilioni 231.6 mwaka 2008/09. Hii ndiyo Wizara iliyoongezewa bajeti inayokaribia kufikia asilimia 50. Kipaumbele katika sekta ya maji ni kuboresha upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya kawaida na umwagiliaji.

-kipaumbele cha sita ni Wizara ya Nishati na Madini ambayo hata hivyo, bajeti yake imeporomoka kwa asilimia 24.6 kutoka Sh. bilioni 378.8 mwaka huu hadi Sh. bilioni 285.5 mwaka ujao. Akifafanua sababu za bajeti ya Wizara hiyo kushuka, Waziri Mkulo alisema ni kutokana na kumalizika kwa mikataba ya kuzalisha umeme kwa makampuni matatu ya kukodi ambayo ni Dowans, Alstom Power Rental (APR) na Aggreko. Alisema kipaumbele cha Wizara kwa mwaka 2009/10 ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme mijini na vijijini. Hata hivyo, alisema theluthi moja ya bajeti hiyo inatarajiwa kutoka kwa wafadhili.


CHANZO: NIPASHE 05-june-2009

Dimitar Berbatov to shine next season

Berba tipped for starring role
Teddy Sheringham is tipping Dimitar Berbatov to have a bigger impact at Old Trafford in his second season as a United player.

The Bulgarian striker bagged 14 goals and countless assists in his maiden Reds campaign, but is still to win over everybody after commanding a transfer fee in excess of £30million. Having trodden the same path from Tottenham, and taken time to settle as a United player, Treble-winning striker Sheringham expects Berbatov to convince his doubters next term.

"He is an outstanding player," Sheringham told the Manchester Evening News. "Sometimes it takes people longer to fit in at a club in terms of the lifestyle and the football, which is probably what’s happened to him.

"But I’ve watched him and I’ve every confidence he will be even better next season. I’ve seen him be outstanding for Tottenham and I’m sure he will be again."

Berbatov's equanimity in possession is in stark contrast to the likes of firebrand forwards like Wayne Rooney and Carlos Tevez, but Sheringham - never known for blistering pace himself - deems it harsh to compare the Bulgarian to his all-action colleagues.

“I was very similar to Berbatov in terms of the way I looked as a player,” he said. “I didn’t look like I was running around either. But just because he is not like Rooney or Tevez doesn’t mean he doesn’t work."


source: www.manutd.com 04/06/2009 07:00, Report by Steve Bartram

Thursday 4 June 2009

'Live within your means!'

'Economic recession?
Stop all fantasy spending and start living within your means'

-Jeff Randall, Sky News (mon.-thurs. 19:30 BST)

R/Post sasa mara 2 kwa wiki

Juni IV, MMIX
Baada ya kuzorota kwa mauzo, wachapishaji wa gazeti la kila siku (jumatatu hadi Ijumaa) Reading Post wameanza utaratibu wa kuchapisha gazeti hilo kwa siku mbili tu kwa badala ya tano. Hii inatokana na hali ngumu kibiashara inayoyakabili magazeti mengi nchini Uingereza.
Mauzo ya magazeti mbalimbali yamekuwa yakishuka kila siku kutokana na hali ngumu ya uchumi kwa wasomaji na watangaza biashara kupitia magazeti hayo. Biashara na huduma mbalimbali za kijamii au kiuchumi zimedorora sana na hivyo kuathiri biashara ya magazeti.
Magazeti hutegemea sana matangazo ya biashara kimapato, na kipindi hiki ni kigumu kwa kila shirika au kampuni kibiashara. Hali inazidi kuwa mbaya hasa pale magazeti yanapopata ushindani kutoka kwa teknlojia ya utandawazi (internet). Biashara sasa hutangazwa mtandaoni ambapo huonwa na watu wengi na kwa haraka zaidi kutokana na ukweli kuwa wateja wengi sasa wanatumia kompyuta na internet ktk kupata habari na pia kwa kununua bidhaa bidhaa mbali mbali. Haya yote ni maendeleo ambayo yanasaidia ktk 'kuua' kizazi cha magazeti (print media).

Miaka minne iliyopita gazeti la Reading Post lilikuwa linauzwa kwa pensi 25 (25p). Hadi juma lililopita ktk toleo lake la mwisho la kila siku, nakala moja ilikuwa inauzwa 40p. Ktk toleo lake la kwanza jana nakala moja ilikuwa inauzwa kwa 20p na toleo la kesho Ijumaa litakalojulikana kama 'getreading' litauzwa kwa 40p na pia litasambazwa bure ktk nyumba zote za wakazi wa Reading.

Washindani wa Reading Post, Reading Chronicle nao wana wakati mgumu. Hivi karibuni walifanya mabadiliko makubwa kiutawala ktk kupunguza gharama. Walipunguza wafanyakazi na kuondoa/kuunganisha vitengo vingi. Aidha walibinafsisha baadhi ya huduma kwa wakandarasi ambao hulipwa kwa mkataba (badala ya kuwa wanfanyakazi wa kudumu). Reading Chronicle wana gazeti moja kubwa la kila wiki siku ya Alhamis ambalo huuzwa kwa 60p kwa nakala moja. Nao mauzo yao sio mazuri. Kadhalika wana magazeti ya bure ambayo husambazwa kwa kila nyumba Reading na vitongoji vyake (Winnersh, Wokingham, Lower Earley, Earley, Woodley, na sehemu za Sandhurst, Crowthorne, Slough, Windsor, Maidenhead n.k.) ktk siku za Jumatano. Magazeti yao ya bure hujulikana kama 'Midweek'.

AON: Man Utd shirt sponsor 2010-14

Future shirt sponsor unveiled
Manchester United today announced that it has reached a significant global partnership and principal sponsorship agreement with Aon Corporation, the world’s leading risk advisor and human capital consultant, to take effect from the start of the 2010/11 season. Terms of the partnership were not announced.

As part of the sponsorship agreement, the Aon brand will feature on the world-famous Manchester United shirt for four years. Announcing the deal, Manchester United chief executive David Gill said, “We are delighted to be entering such an important relationship with a company of the stature of Aon and to have its logo adorn our shirts from the start of the 2010/11 season.

"We look forward to being closely aligned with the world leader in risk management, a firm which shares our values and is an exciting partner for Manchester United. Today's announcement clearly strengthens our position as one of the biggest clubs in world football."

"It is a unique opportunity when two leaders in their respective fields can come together in a partnership such as the one we are announcing today,” added Greg Case, president and chief executive officer of Aon.

“Manchester United has one of the most recognised sports brands in the world. David and his team are all about winning and about excellence; the same holds true for the Aon team. We play to win in our business, and that is why we believe this partnership will create tremendous benefits for both organisations worldwide.

“While we are delighted that our brand will be showcased to over 330 million fans of Manchester United as well as the countless followers of football worldwide, we also are extremely excited about the opportunity to maximise the value of this partnership globally.”


source: www.manutd.com, 03 June 2009.

Watoto wa teknolojia

Juni IV, MMIX
Jana nilipokea ujumbe wa maneno kwa simu ya mkononi kutoka kwa mwanangu ambaye ameanza masomo ya shule ya msingi hivi karibuni. Nilishangaa sana.

Siku hizi watoto wadogo kabisa nchini wanaweza kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa, mfano kompyuta, simu za mkononi n.k. bila shida. Bila shaka haya ni maendeleo ya kutia moyo.

Sio muda mrefu ujao, suala la ujinga litakuwa sio kutojua kuandika na kusoma bali kutojua kutumia kompyuta. Na hii ndio itakuwa vita mpya kitaifa! Miaka ya 1970, Mwalimu aliendesha kampeni ya 'Jifunze Kusoma, Wakati ni Huu'. Mimi nadhani huu ni wakati wa kuzindua kampeni mpya ya kujifunza kutumia 'teknolojia ya habari' ya kisasa.

Ikumbukwe kuwa kizazi cha watu wazima wa sasa wameanzia ukubwani kuziona na kuzitumia teknolojia hizi!

Wednesday 3 June 2009

Vijana wadogo wasaidiwe

June III, MMIX
Natoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa watoto wote wanaoanza shule za msingi waruhusiwe kuendelea hadi kidato cha nne. Baada ya hapo, kwa wale ambao hawatapata nafasi kujiunga na kidato cha tano ama vyuo vingine (vya afya, kilimo, elimu n.k.) wapewe nafasi kujiunga na vyuo vya ufundi (VETA) moja kwa moja. Kwa maana hii karibu watoto wote watakaohitimu kidato cha nne watakuwa wamepata nafasi ya kujiandaa na maisha yao ya baadaye.

Hawa watoto watakapomaliza masomo/mafunzo yao popote pale watakapokuwa wameendelea (kielimu au ktk stadi mbalimbali kitaaluma), wataweza kujiajiri na hivyo kuwa walipa kodi wa miaka ijayo. Kinyume chake, kwa mtindo wa sasa, vijana kukaa mitaani kwa kisingizio cha kukosa ajira ni hatari kwa Taifa kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Vilevile natoa ushauri kuwa vijana wote watakaojiunga na mafunzo ktk vyuo vya VETA wadhaminiwe na serikali za mitaa kwa ushirikiano na serikali kuu. Kwa kweli serikali zetu zina uwezo wa kuwasaidia hawa watoto hawa ktk kujiandaa na maisha yao ya baadaye.

Tuesday 2 June 2009

Baraza la Mwalimu

June II, MMIX
Miaka ya 1980 mwanzoni (miaka 5 kabla ya Mwalimu kustaafu 1985) nilianza kutambua baraza lake mawaziri.
Hapa nawakumbuka wachache kama ifuatavyo;

Aboud Jumbe Mwinyi - Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar

Cleopa David Msuya - Waziri Mkuu 1980 (pia Fedha, Biashara na Viwanda)
Edward Moringe Sokoine - Waziri Mkuu 1983
Salimu Ahmed Salim - Waziri Mkuu, 1984 (pia Mambo ya Nje, Ulinzi na JKT)

Ali Hassan Mwinyi - Waziri wa Maliasili na Utalii 1982 (pia Rais wa muda Zanzibar 1984)

Ali Nasoro Moyo -?

Abdalla Twalipo - Ulinzi

John Malecela - Mawasiliano na Uchukuzi, (pia Mkuu wa mkoa Iringa)

Mwingira - Mawasiliano na Uchukuzi, mkuu wa mkoa Mara

Al Noor Kassum - Maji na Nishati

Getrude Mongella - Maliasili na Utalii (pia waziri asiye na wizara maalumu)

Amir Habib Jamal - Biashara na Viwanda (pia fedha)

Ibrahim Kaduma - Kilimo?? (pia mwenyekiti bodi ya mkonge)

Herman Kyanzi Kirigini - Mifugo (ofisi ya Rais)

Timothy Apiyo - K/mkuu ofisi ya Rais

Julie Manning - Sheria na Mwanasheria Mkuu

Tabitha Siwale - Elimu ya Taifa

Kate Sylvia Magdalena Kamba - ?

Muhidin Kimario - Mambo ya Ndani

George Clemence Kahama - ?

Basil Pesambili Mramba - Biashara na Viwanda, Fedha

Samuel Sitta - ujenzi

Venance Ngula - Naibu waziri Fedha

Benjamin William Mkapa - Mambo ya Nje (pia Habari na Utamaduni na balozi Marekani)

Mustapha Nyang'anyi - ?

Joseph Warioba - Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu

Rashid Mfaume Kawawa - Waziri asiye na wizara maalum

Said Natepe - Mambo ya Ndani

Timothy Shindika - ?

Jackson Makweta - Kilimo, Elimu ya Taifa, Madini??