Friday, 20 February 2009

Nyumba 75,000 kutwaliwa na mabenki!

Nimeona habari leo kuwa waingereza wengi mwaka huu wanaelekea kupoteza nyumba zao kutokana na kukabiliwa na ukata (ukapa?) na hivyo kushindwa kulipa madeni yao ya kila mwezi. Waingereza walio wengi hukopa hela kutoka taasisi za fedha (benki) kwa ajili ya kununua nyumba za kuishi na baadae hukatwa kila mwezi kulingana na ukubwa wa deni.

Ugumu wa maisha umepelekea wengi wao kutolipa deni kwa miezi mitatu mfululizo iliyopita. Hicho ni kiashirio kwa mabenki kuchukua hatua zaidi ili kurejesha fedha zao, na inahofiwa kuwa nyumba 75,000 ziko mbioni kutwaliwa na kunadiwa na mabenki kwa ajili ya kugomboa deni lao. Maisha ya watu hao yanategemewa kuwa magumu hasa baada ya kupoteza makazi yao. Hilo ni ongezeko la asilimia 60 ukilinganisha na takwimu za mwaka jana ktk kipindi kama hiki. Habari hii ni kwa mujibu wa kipindi cha 'breakfast', bbcone-tv 20/02/2009.

No comments: