Thursday, 19 February 2009

1/7 ni 'wakuja'

Takwimu zilizotolewa juzi uingereza zinasema kuwa kuna wafanyakazi wapatao milioni 4 kutoka nje ya uingereza ambao wanafanya kazi ktk nchi hiyo. Hii ni sawa mfanyakazi mmoja kati ya saba, ya wanaofanya kazi, anatoka nje ya uingereza.

Tayari malalamiko yametanda ktk baadhi ya vyombo vya habari kutaka mipaka idhibitiwe na kutoruhusu watu kuingia nchini kwao na kuchukua kazi ambazo zingefanywa na raia wa nchi.

Hii yote imeletwa na matatizo ya uchumi yaliyoikumba dunia hivi sasa -kwa sababu wafanyakazi hao walikuwapo tangu zamani ila wamekumbukwa baada ya watu (wazawa) kupoteza kazi zao hivi karibuni.

Kusema kweli siku hizi kuna watu wengi sana wanazunguka mijini na mitaani (hasa ktk high streets) hawana pa kwenda wala cha kufanya. Na siku hizi huwezi kutofautisha siku za weekend, siku-kuu na siku za kawaida maana uwingi wa watu siku za kawaida za juma umeongezeka.

Bahati njema ni kwamba raia wa hapa kama hawana kibarua huwa wanadai malipo (benefits) kutoka serikalini, kwa hiyo anayeumia kwa sasa ni serikali yao na ndio maana inahaha kutafuta nafasi za kazi kwa raia ili isiendelee kuwalipa 'benefits'.

Kwa 'wakuja' kama hawana job wanaipa 'fresh' maana hawana haki kupata 'benefits' pamoja na kwamba wanalipa kodi na bima ya taifa (n.i.) kama kawaida.

No comments: