Tuesday, 17 February 2009

Tujihadhari na Nyama nyekundu

Utafiti umeonyesha kuwa nyama ya ng'ombe, kondoo, nguruwe n.k. husababisha magaonjwa ya saratani ya; matiti, ... (prostate) na tumbo. Pia nyama hizo ambazo hujulikana kama red meat zikiwa na mafutamafuta husababisha magonjwa ya moyo na kiharusi. Tunapotumia nyama ni vizuri kuondoa tabaka la mafuta ili kujiepusha na madhara hayo kiafya.

Sio vibaya kula nyama, ila tunachoshauriwa ni kuwa isiwe kila siku na kila mlo (kula nyama mara 2 kwa wiki sio vibaya).

Wataalamu wa afya na vyakula wanatushauri kutumia nyama za kuku na samaki kwa wingi huku tukipunguza matumizi ya nyama nyekundu.

Pia tunashauriwa kutumia matunda na mboga za majani ili kujikinga na saratani na magonjwa ya moyo.


Habari hii ni kwa mujibu wa gazeti la daily-express la J'nne Februari 17, 2009 ukurasa wa 7.

No comments: