Saturday, 28 February 2009

'Ghost highstreets'

Inahofiwa kuwa maeneo ya mijini (highstreets) Uingereza inaweza kugeuka 'mahame' endapo hali mbaya ya uchumi itaendelea kama ilivyo sasa.

Wakuu wa halmashauri za miji za Uingereza wanasema hali sio nzuri kwa wenye maduka kwa vile biashara imedumaa kabisa siku hizi. Watu hawanunui bidhaa madukani na hivyo kuzorotesha mapato ya kibiashara na pia serikalini kupitia kodi za mauzo.

Tayari maduka makubwa kadhaa yameshafunga biashara zao (mfano Woolworths, Adams, Zavvi n.k.) na wale wanaoendelea na biashara wanaendesha zoezi la kupunguza gharama za uendeshaji kwa kupunguza wafanyakazi pamoja na kufunga baadhi ya matawi ya biashara ambayo hayana faida.

No comments: