Wednesday, 5 May 2010

'Wewe Mungu Ni wa Ajabu' - Mchungaji Abiudi Misholi

...................................
Wimbo: Wewe Mungu Ni wa Ajabu
Muda: Dakika 7 Sek. 46
Wimbo wa: 1 kati ya nyimbo 9
Mtunzi/Mwimbaji: Mch. Abiud Misholi (Faraja Band)
Album: Shuka Bwana Shuka (Nyimbo Za Kuabudu)

Mwandishi: Mosonga (Pamoja na msaada kutoka kwa Mch. Abiudi Misholi tar. 15/05/2010 ktk kuboresha mstari mmojawapo).
......................................


Wewe Mungu ni wa Ajabu, Fadhili zako ni za Milele.
Unastahili kupewa sifa, kwa kila hali na kila sababu.
Haleluya.


Nikifikiri maisha yangu, Mapito ninayopitia.
Taabu na shida, Kero nazopitia.
Ndipo ninapojua mimi, Wewe ni Mungu.
Ndipo nnapojua mimi, Wewe ni Baba.

Ukasema Abiudi, Nenda kanitumikie.
Nikasema siwezi, Sitaki Kukutumikia.
Dada yangu mgonjwa, Nyumba yenye majaribu.
Mama yangu huzuni kutwa, Mimi niache!

Ukaanza kunitesa Mungu, Pasipo sababu.
Ukaharibu biashara zangu, na kila nilolifanya.
Nikawa na maisha magumu, kula kwa taabu.
Madeni ni mengi, Sabuni taabu.
Nikataka kujiua, Maisha magumu.
Sina amani, vidonda vya tumbo.
Usiku silali mimi, Mawazo tele.
Maisha magumu mimi, mimi nifanyeje.

Ukajibu usijue, niende kukutumikia.
Na mimi nikakubali, kwenda kukutumikia.
Nikaenda kijijini mimi, kufungua kanisa.
Na mke wangu cheupe, na Noah mwanangu.

Oh! Nikikumbuka, nafika mbali.
Haleluya.


Nikafikiri matatizo, sasa yatakwisha.
Lakini badala yake, Matatizo yakaendelea.

Wewe ni Mungu ee, Mungu nakuabudu.
Wewe ni Baba, Sikuachi hata iweje.

Siku moja mke wangu, akiwa mjamzito.
Uchungu umemshika, Pastor ana 'Mia Hamsini'!
Mke wangu kwa uzuri, anasema mume wangu.
Nenda kakope pesa, nipeleke hospitali.
Nikajibu siendi, nimechoka kuombaomba.
Pesa za malalamiko, pesa za masimango.
Kama Mungu Ametuita, mke wangu tusubiri.
Kama Mungu Ametuita, Yeye Atutetee.
Saa kumi za usiku, mke wangu anajifungua.
Mbele ya macho yangu, Daktari mimi mwenyewe!

Wewe ni Mungu tuu, Wewe ni Baba
Haleluya!
Wewe ni Mungu, Wewe ni Baba

Ndugu yangu nataka nikuambie neno moja.
Mungu kumuelewa ni kazi sana, lakini endelea kumwabudu.
Usinung'unike!
Muheshimu na kumtukuza.
Iko siku Atakujibu.
Haleluya!


Wewe ni Baba. Wewe ni Baba. Wewe ni Baba. Wewe ni Baba.

Wewe ni Baba. (Wewe ni Mungu)
Wewe ni Baba. (Wewe ni Mungu)
Wewe ni Baba. (Wewe ni Mungu)
Wewe ni Baba. (Wewe ni Mungu)

Mungu wa Elia. (Wewe ni Mungu)
Mungu wa Isaka. (wewe ni Mungu)
Mungu wa Yakobo. (wewe ni Mungu)
Mungu wa Mwalengo (Wewe ni Mungu)
Mungu wa Misholi. (Wewe ni Mungu)
Mungu wa Jeremia. (Wewe ni Mungu)
Mungu wa Maliseli. (Wewe ni Mungu)
Mungu wa Licheli. (Wewe ni Mungu)

Ayubu alipata mateso,
Ayubu alipata Shida.
Mimi sio wa kwanza.

Mitume na manabii walipata taabu,
Walipata shida, lakini waliendelea kusema wewe Mungu ni Baba.
Katika matanuru ya moto wakasema Wewe Mungu ni Baba.
Wakawekwa magerezani, wakasema Wewe Mungu ni Baba.
Hawajaacha kukiri, kila mara wakasema Wewe ni Baba.

Mke wa Ayubu alicharuka, akasema Wewe sio Mungu.
Wewe Mungu ni Nani, Mungu gani mkorofi.
Mungu Umeua watoto wangu,
Mungu Umeua, Umeua mifugo yetu!
Mungu Unamtesa mume wangu,
Ayubu kufuru ufe mume wangu

Lakini Ayubu akasema Huyu ni Baba tu!
Hata iweje Huyu ni Baba!
Hata tutesekeje Wewe ni Mungu.
Tupate shida, tusimangwe, tuchekwe, tudharauliwe - Bado Wewe ni Mungu.
Wewe ni Baba, Wewe ni Baba tu!

Usimwache Mungu ndugu yangu! Hata ukitengwa.
Hata ukitesekaje, Yeye ni Baba Yako tu!
Mshukuru, Mwimbie
Tena saa nyingine hata Akikulaza njaa - ndio kwanza piga pambio.
Uko gerezani, Fanya kama Paulo na Sila. Piga Makofi.
Yeye ni Baba tu! Hata Iweje.
Haleluyah!


Wewe ni Baba, Wewe ni Baba, Wewew ni Bab, Wewe ni Baba.
Wewe ni Baba, Wewe ni Baba, Wewe ni Baba, Wewe ni Baba.
..................................................

MWISHO!

............

Shukurani kwa Mch. Abiudi Misholi, kwa kunisaidia maeneo fulani ktk huu wimbo yaliyokuwa yananitatiza wakati naendelea kuuandika huu wimbo kutoka kwenye CD ya album yake.

Feliz CumpleaƱos!!!!

........................
Dear Mpendwa wetu, Baba Tezy.

On this special day in our Family, we would like to say,


HAPPY BIRTHDAY to you!!!

We love you, our dady and hubby!

From,
Tezy and Mama Tezy

..........................