Friday, 15 May 2009

Hii sio haki

Ijumaa mei 15, 2009
“.... Pombe zote hakuna kuuzwa katikati ya wiki isipokuwa Jumapili na siku za sikukuu, ni lazima turudishe nidhamu ya kilimo bora, kilimo cha kufa na kupona,” alisema Waziri Mkuu (Mizengo Pinda).

Kama pombe anazozungumzia mheshimiwa WM ni halali, basi hakuna haja kuwapiga vita wajasiamali wanaopika pombe hii. Hii ni biashara ya mtu inayompa kipato cha kuhimili gharama na makali maisha kila siku.

Waziri mkuu anapopiga marufuku pombe, hakomoi wanywa pombe bali pia wapika pombe ambao hutegemea kipato kupitia hiyo biashara.

Enzi za kulazimisha watu kulima ilishapitwa na wakati. Serikali isaidie ktk kuandaa au kuweka mazingira ya kuvutia kilimo vijijini ili mwananchi aweze kuwekeza mali, nguvu na muda wake ktk kilimo kwa hiyari yake. Kadhalika serikali iwe na mkakati endelevu wa kutoa ruzuku ktk bei za pembejeo za kilimo ili wananchi wajikomboe na kuinama shambani kwa kutumia jembe la mkono au la ng'ombe.

Sio busara kuswaga watu kwenda shambani pasipo kuwaandalia mazingira mazuri ya kupenda kilimo. Ktk hotuba ya WM sikuona anataja suala la mapinduzi ya kilimo kwa utumiaji wa mashine za kisasa ili kuwarahisishia wananchi utendaji kazi za shambani.

Ni nani apendaye kupinda mgongo shambani kwa kutumia zana za miaka ya sitini? Na kwa serikali yetu, acheni kuwatisha wananchi, cha muhimu ni serikali kuwasaidia ktk kufanya mapinduzi ya kilimo.

Hapo ndipo kila mtu atapenda kwenda shambani.

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Amani, Heshima na Upendo kwako Ndugu.
Wanachonishangaza Ndugu hawa wakuu ni namna ambavyo wanaangalia "nje ya ulingo waliomo" ambao ndio uliooza.
Hakuna atakayegoma kukaa kijijini kama huduma zote muhimu zitapatikana. Kama kutakuwa na mazingira ya kumfanya aweze kuuza japo bidhaa zake. Lakini wanaendekeza siasa na kujiandaa kusikika kuliko kutekeleza. Hashangai kwanini watu wanauza pombe badala ya shughuli ambazo wao wanaweza kudhani ni za kuwapatia kipato zaidi? Hawaoni kwanini watu wamechoka kuwasiliza, wanawazomea na kuwaona waongo kama niwaonavyo mimi. Ni kwa kuwa wanasema wakijua TBC iko pale lna hakuna atakayehoji wala kutaka ufafanuzi wa ahadi walizotoa wiki mbili zijazo.
Ni upuuzi kuona Waziri Mkuu hamuwajibishi mkuu wa sehemu hiyo (awe wa wilaya ama mkoa) kujua ni kipi kinachokwamisha maendeleo ya wananchi.
Ni lazima tuwe na mikataba, kuwa mtu anapokubali kuchukua kazi kama ya ukuu wa mikoa awe na ahadi ya kufanya vitu kadhaa ndani ya muda fulani, na akishindwa na aachie ngazi. Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ni kati ya watendaji wabovu zaidi nchini Tanzania.
Waziri aanze na wasaidizi wake kabla hajawaendea wale walioshindwa kuwezeshwa wakaamua kujiwezesha.
Shukrani kwa kazi njema