Wednesday, 6 May 2009

Ucheshi wa kiafrika

Wed. May 06, 2009
Ni kawaida kuona viongozi (hasa marais) kutoka nje ya nchi wanapotutembelea, hukaribishwa na wenyeji wao (rais wetu, makamu, waziri mkuu na wasaidizi wao) kwa ucheshi na ukarumu wa hali ya juu!

Pale uwanja wa ndege huwa kuna watoto chipukizi tayari kuwavisha mashada wageni wetu na pia vikundi vya ngoma, sanaa na utamaduni huwepo kuwaburudisha wageni.

Barabarani watu hujipanga msururu wakiwa na bendera za nchi yetu na za mgeni husika! Shamrashamra huendelea njiani kote hadi ikulu ambako nako hupokewa na vikundi mbalimbali na wenyeji zaidi kwa furaha na chereko!

Vyombo vya habari nchini (TV, magazeti na redio hutangaza habari za ujio wa mgeni wetu nchi nzima!

Furaha na chereko kwa mgeni huendelea muda wote anapokuwa nyumabani kwetu (nchini) hadi anapoondoka na kutia mguu kwenye ndege na kupaa, huwa tunampungia mkono na kumtakia safari njema!

Kwa kweli ukarimu wetu waafrika ni wa kweli.

Kwa upande wa pili, viongozi wetu (rais, makamu na waziri mkuu) wanaposafiri nje ya Afrika hali huwa tofauti. Kwanza Rais wetu anaweza asipokelewe na mwenyeji wake uwanja wa ndege. Pili hakuna nderemo wala shamrashamra zozote na ataelekea hotelini kwake moja kwa moja. Anaweza kuonana na mwenyeji wake kwa dakika chache au akiwa na bahati masaa machache tu, na hawaonani tena! Vyombo vya habari ndio usiseme hata havitaji au kutangaza ujio wa Rais wetu huku ughaibuni!

Mungu ametujalia wema na ukarimu, na nina uhakika wenzetu wanautamani!

No comments: