Tuesday, 26 May 2009

Nani aitangaze nchi yetu nje?

Ni kawaida yetu sisi kulaumu serikali zetu hazifanyi jitihada yoyote kuitangaza nchi yetu ughaibuni (nchi za nje). Tumekuwa tunalaumu pia wizara husika ya Utalii ni kwa nini haitangazi vivutio vya utalii vilivyoko nyumbani n.k.

Kwa upande wangu naona suala hili ni la pande zote. Sio la serikali pekee. Hata wale wanaopata nafasi ya kufika au kuishi huku japo kwa muda kidogo, no wana wajibu pia kwa kiwango chao. Naweza kusema ni wadau wa ktk kutangaza nchi yetu pale walipo na kwa uwezo walio nao.

Kwa bahati mbaya, ninashangaa sana kuona hawa wadau (watanzania walio ughaibuni) hawatekelezi linalowahusu ktk kuitangaza nchi.

Natoa mfano mdogo tu.
-Je watanzania walioko nje (wa kiume na kike) wanavaa mavazi gani? Wanavaa vito gani?
-Je wanasikiliza muziki wa aina gani majumbani kwao na vyombo vyao vya usafiri (ndani ya magari yao)?
-Majumbani kwao ukutani kuna picha za mandhari za wapi?

Mara nyingi utakuta tunasikiliza miziki ya nje hadharani, mavazi ya mitindo ya nchi za nje, picha za huko Marekani n.k.

Huu ni wakati wa kuamka ili tuweze kuchangia ktk kuitangaza nchi yetu hasa kwa kupitia utamaduni wetu na mali asili zetu! Kwa kufanya hivyo tutaweza kuiweka nchi yetu hadharani, maana sisi ndio tulioko mitaani na watu wanakutana nasi kila siku. Sisi ni kioo cha nchi yetu, na ndio maana nasema kuwa mchango wetu ni mzito zaidi kuliko matangazo kwenye luninga na majarida mbalimbali.

No comments: