Saturday 9 May 2009

Hali ngumu ya Uchumi: Bunge lifupishwe

Saturday May 09, 2009
Bunge la Jamhuri ya Muungano liko mbioni kukutana ktk marathoni ya vikao vya kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2009/10.

Kama wote tujuavyo, hiki ni kipindi kigumu sana kiuchumi duniani kote. Ni vizuri viongiozi wetu na wawakilishi wetu wakazingatia hali tuliyonayo na kuchukua hatua za kusaidia kupunguza makali ya uchumi.

Mojawapo ya hatua za kuchukua ambazo ziko ndani ya uwezo wetu ni kufupisha urefu wa vikao vya Bunge. Kwa kawaida vikao vya bajeti huchukua miezi miwili (Juni hadi Agosti kila mwaka).

Napendekeza kwa waandaaji wa ratiba za
1. hotuba za mawaziri kuwasilisha bajeti na
2. muda wa waheshimiwa wabunge kujadili bajeti hizo,
zifupishwe kwa asilimia 10 au zaidi.

Hotuba kuu ya waziri wa fedha na wa mipango kuhusu hali ya uchumi wa nchi ndizo zipewe muda wa kawaida, lakini hotuba zote za wizara zinazofuata zifupishwe kama nilivyopendekeza kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.

Haitakuwa uamuzi wa busara kutumia gharama kubwa kuendesha vikao wakati huduma muhimu kwa wananchi zinayumba kwa kukosa fedha za kuziendesha. Kama wananchi wanaambiwa wafunge mikanda kila siku, inakuwaje wakubwa waendelee kulegeza ya kwao?

Kila mtanzania ana wajibu wa kubana matumizi ktk nafasi yake aliyoko, na nyie wawakilishi wetu fanyeni vivyo hivyo!

No comments: