Saturday 21 June 2008

Ushamba, fasheni na msimamo!

Si kipindi kirefu kilichopita mtu akionekana na mfuko wa plastic uliotumika anaonekana mshamba. Siku hizi wataalamu wanasisitiza kutumia mifuko ya plastic (rambo) mara kwa mara ili kutunza mazingira.
Nani angetembea barabarani na viroba (mifuko ya gunia), mtaa mzima wangemzungumza kuwa mtu wa kuja. Lakini hivi sasa ndio imerudi iko ktk fasheni - eti wanaiita 'bio-degradable'! Si ndio ileile tuliyokuwa tunachekwa nayo lakini?

Je ungeshona nguo kwa sindano ya mkono hiyo nguo ungeivalia wapi? Lakini unaonaje siku hizi si makoti yanatoka kwa staili ya ushonaji wa mkono!! Au ukivalia nguo ndani nje, inakuwaje. Siku hizi zinashonwa ndani nje na inakubalika!

Vipo vitu vingi vizuri ambavyo watu wanaacha kufanya eti kwa sababu ni vya ki-shamba.
Muda si muda unakuta ndio vipo ktk chati. Lakini vinakuwa ktk chati kwa sababu fulani (mtu maarufu) kaonekana navyo.

Ni kwanini mtu aache kufanya mambo yale aliyozoea kufanya au yale yanayomfaa ktk maisha ya kila siku kisa ataonekana mshamba? Lakini mtu kama Beckam au Naomi Campell akiyafanya yaleyale 'ya kishamba' - inaonekana ni fasheni!

Cha msingi ni kuwa na msimamo na utaratibu wako kimaisha na pia kujali utamaduni wako kiustaarabu!

No comments: