Thursday 12 June 2008

Bei ya vyakula juu!

Bajeti 2008/09: Mambo Magumu!
(SOURCE: Alasiri, 2008-06-11 18:01:14 Na Sharon Sauwa)
Wakati Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Mhe. Mustafa Mkulo akitarajiwa kuwasilisha bajeti ya mwaka 2008/09 katika mkutano wa 12 wa Bunge kesho (alhamis), bei ya vitu imepanda maradufu kulinganisha na kipato na hivyo kuwafanya wananchi wengi kuwa na maisha magumu zaidi.

Mwandishi amebaini kuwa mbali na pesa nyingi wanazolipa wakazi wa Jijini kutokana na kupanda kwa gharama za usafiri, pia vyakula, huduma za matibabu, umeme na hata vifaa vya ujenzi vimepanda mno kwa namna inayofanya maisha yawe magumu zaidi.

Bei za vyakula na bidhaa/huduma mbalimbali kulingana na uchunguzi wa gazeti 'Alasiri':
Nauli ya daladala hutozwa kati ya Sh. 250 hadi Sh. 1,000 kulingana na eneo na umbali wa safari yenyewe, katika baadhi ya maeneo mengi Jijini.
unga wa mahindi huuzwa kati ya Sh. 700 hadi 800 kwa ujazo wa kilo moja.
Mchele huuzwa kati ya Sh. 900 hadi Sh. 1,300,
maharage Sh. 1,200 hadi Sh. 1,500
mkaa kipimo kimoja kikiwa kati ya Sh. 700, 1,000 na hadi Sh. 1,200 kwa maeneo kama ya Kimara Bonyokwa.
vitunguu na nyanya ambavyo vyote, huuzwa kwa wastani wa Sh. 100 kwa kimoja, au Sh. 400 kwa fungu lenye nyanya tatu hadi nne au vitunguu vya idadi hiyo
bamia fungu likiuzwa kati ya Sh. 100 na 300.
nyama ya kawaida imekuwa kimbilio la wengi kwa sasa, kutokana na ukweli kuwa yenyewe imeendelea kuuzwa kwa wastani wa Sh. 2,800 hadi 3,500, kulingana na eneo.
Sukari nayo huuzwa kwa Sh. 1,000 hadi Sh. 1,200 kwa kilo,
mafuta ya kula huuzwa Sh. 150 kwa kipimo kidogo kabisa kwenye maeneo kama ya Tandale na Buguruni huku fungu la bamia ni sh 100.
dagaa wanaopendwa zaidi toka Kigoma huuzwa kwa kati ya Sh. 7000 hadi sh 9,000,
nanasi Sh.1,000 na 1,500,
embe dodo sh. 500 hadi 700 na
machungwa Sh.100 hadi 150.

maji yanayouzwa kwenye madumu katika maeneo yenye shida ya maji huuzwa kwa kati ya Sh. 300 hadi Sh. 500 kwa dumu moja la lita 20.
mafuta ambayo hutajwa kuwa ni sababu kubwa zaidi ya kupanda kwa maisha imeendelea kupanda siku hadi siku ambapo sasa, katika baadhi ya vituo vya mafuta, dizeli huuzwa kwa Sh. 1,950 kwa lita, Petroli Sh. 1850 na mafuta ya taa Sh. 1,300.

Bei ya samaki imekuwa haishikiki, ingawa hushuka kidogo pale wanapovuliwa kwa wingi wakati bahari inapotulia na giza kutawala usiku.

No comments: