Monday 30 June 2008

Kituo cha Polisi Kati ( ni tafsiri sahihi?)

Mara nyingi vyombo vingi vya habari hutangaza tafsiri ya maneno 'Central Police Station' kama kituo cha Polisi cha 'Kati'.

Mimi huwa nafikiri kuwa tafsiri sahihi ni kituo 'Kikuu' cha Polisi.

Mfano:
Kamati Kuu ya CCM huwa ni 'CCM's Central Committee'
Benki Kuu ni 'Central Bank', n.k.

Inakuwaje kiitwe kituo cha kati? Au ndio tafsiri sahihi? Ningependa kuelemishwa kuhusu hiyo tafsiri, maana inawezekana mimi ndie nimepitiwa kidogo!

..........................................................
KWA MFANO TAZAMA HII HABARI:

Mintanga akamatwa na polisi
(Source: Nipashe, 2008-07-07 09:03:21. By Somoe Ng'itu)
Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Shaaban Mintanga kutokana na kudaiwa kuhusika na sakata la mabondia wa hapa nchini kukamatwa Mauritius kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya.

Mintanga, ambaye awali alikuwa Rais wa Chama cha Ngumi mkoa wa Dar es Salaam (DABA) anashikiliwa katika kituo cha Polisi Kati.
.....................................

No comments: