Monday 2 June 2008

Shirikisho A/Mashariki: ulikuwa ni utabiri au ukweli?

Tarehe 04/12/2006 niliwahi kuisema Kenya juu ya maendeleo yao kidemokrasia kwamba ni kikwazo tosha kutoruhusiwa kuwa mwanachama wa shirikisho (wakati nikijenga hoja kuwa huu sio wakati muafaka kuanzisha shirikisho la Afrika Mashariki).

Na kweli wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana (2007) maoni yangu yalipata nguvu zaidi, maana wakenya wenyewe walithibitisha dukuduku langu la wakati huo lilikuwa na ukweli! Ziliibuka vurugu na mapigano ambayo yaligeuka kuwa mauaji ya raia mithili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe tulivyosikia au kuona ktk vyombo vya habari huko Somalia, Burundi na Rwanda!

Nilisema hivi: "Kenya demokrasia ni finyu sana na juzijuzi wameshindwa kutuletea wabunge 9 tu wa bunge la A. Mashariki na hadi sasa kesi iko mahakamani. Sasa wana ubavu wa kutoa wabunge wa bunge hilo la shirikisho? Tumeona hawana ubavu huo!! Uongozi wao si wa uwazi, tumeona mawaziri/manaibu waziri wanaachia ngazi" -04/12/2006

Na kweli Kenya hamna ubavu huo wa kutuchagulia wabunge au mnasemaje?

No comments: