Friday, 13 March 2009

Tovuti ya Mwalimu imepotelea wapi?

Tovuti ya Mwalimu Nyerere Foundation ambayo ilikuwa iko ktk mtandao imepotea kinyemela tangu mwaka jana. MNF ilianzishwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1996.

Sijawahi kusikia au kusoma mahali popote ni nini kimesababisha tovuti hiyo itoweke ktk mtandao. Ni matumaini yangu wahusika MNF watashughulikia tatizo lililosababisha kutoweka kwa tovuti hiyo ili irejee hewani. Wananchi tungependa kujua kinachoendelea ndani ya MNF na shughuli zinazofanywa na Foundation ya Mwalimu.

Na njia rahisi ya kuwafikia watu wengi nchini kote au duniani ni kupitia kwenye mtandao. Ingawa zipo njia nyingine za kuwafikia walengwa -mfano redio, television na magazeti - bado njia ya mtandao inasambaa kwa haraka zaidi na kwa gharama nafuu. Kumbuka hata wahisani, wafadhili au watafiti ni rahisi kufuatilia shughuli za MNF kupitia mtandao kuliko hizo nyinginezo!

No comments: