Friday, 27 March 2009

Mwisho wa Mwezi na Bili zake!

Mwisho wa mwezi umewadia. Ni wakati wa furaha -maana kuna kitu kidogo mfukoni!! Lakini furaha ya kupata mshahara inaweza kuwa ya muda mfupi hasa ukizingatia bili za mwezi nazo ndio muda wake kudondoshwa mlangoni.

Kwa walio wengi mshahara wa mwezi kwa wastani ni kati ya Paundi za Uingereza 1,500 na 2,000!

Ukishapokea mshahara wako, toa bili zifuatazo na unachobakiwa nacho ndio ufanyie shuguli zako za pembeni pamoja na kusaidia jamaa kule nyumbani Afrika. Kumbuka mshahara huo hukatwa kodi ya mapato (income tax) asilimia 20, na pia hukatwa bima ya taifa (National Insurance).

Bili zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Kodi ya chumba au nyumba. Kwa wastani chumba kimoja cha single ni £250-280 kwa mwezi, chumba double ni kwenye £300 hadi 350 ukinjumlisha na bili za ndani (mpangaji)

Kodi ya flati vyumba 2 ni kwenye £450 hadi 500, nyumba nzima ni kwenye £700 hadi 800.

2. Bili za maji (miezi 3) na gesi na umeme (miezi 3).

3. Bili za broadband (utandawazi -internet, TV, pamoja na simu ya ndani -landline)

4. TV Licence (kwa mwaka -£131.00 au kila mwezi)

5. Bili za Simu za mkononi (mkataba) kwenye £15 hadi 35 au zaidi.

6. Bili za Mikopo (credit cards na/au personal loans monthly payments) -kulingana na ulivyokopa mwenyewe!

7. Bili ya kodi ya halmashauri ya mji (council tax)

8. Usafiri: Nauli (usafiri wa mabasi/treni) au mafuta ya gari (fuel)

9. Mahitaji ya kimsingi ya binadamu kama vile Chakula

10. Mengineyo

Ukishatoa gharama hizo zote, unajikuta umebakiwa na deni. Kwa hiyo unaanza mwezi unaofuata na mkopo kama kawaida, na maisha yanaendelea.

Ndio maana huku ulaya watu wanaishi kwa mikopo kila siku. Ukweli ni kwamba hela haikaliki mfukoni. Kinachofanya kazi ni plastic cards (credit cards na debit cards kutoka ktk mabenki). Kwa jinsi hii mabenki yanatengeneza faida na watu pia wanafaidika ktk kuweza kumudu gharama za maisha ya kila siku! Bila hivyo Ulaya hakukaliki na wala hakulaliki!

No comments: