Tuesday, 10 March 2009

Kijani ipi ni ya Si-Si-Emu?

Bado sijaelewa rangi rasmi inayotumiwa na Chama Cha Mapinduzi.

Zipo aina nyingi za rangi ya kijani (ambayo inatawala ktk bendera ya chama na mavazi rasmi ktk matukio ya kichama).

Ktk tukio moja unaweza kukuta rangi za kijani kibichi, kijani ya kawaida na kijani iliyopauka zote zimetumika ktk bendera na mavazi ya viongozi wa ngazi za juu. Ukiwaona kwa pamoja unaweza kusema waziwazi kuwa hii sio sare (ingawa wao watasema ni sare ya chama!)

Ingekuwa vema kama wana-ccm wangeamua rangi gani ya kijani ni muafaka ili itumike rasmi, badala ya kuchanganya rangi anuai za kijani.

No comments: