Monday, 30 March 2009

Madona na mradi wa 'kununua' watoto

Kwa mara ya pili mwimbaji maarufu Madona ametinga tena nchini Malawi akitaka 'kununua' mtoto.
Mwenyewe anatumia lugha ya kilaghai ei 'ku-adopt' na kudanganya mamlaka za kisheria Malawi!
Damu ya waafrika inanunuliwa kirahisi hivi, hata baadhi ya wazungu wanapinga hasa ile taasisi ya 'save the children' wanasema mtoto anapaswa kuangaliwa na jamii inayomzunguka na sio kumbadilishia mazingira.
Mimi napinga sana dhana hii ya Madona hata pale alipoenda 'kununua' mtoto wa kwanza.
Wengine wanasema eti mtot amepata bahati, kwa hiyo aachwe akaule huko Marekani!
Ikumbukwa Madona haendi kuchukua mtoto yeyote yule, bali anachukua mtoto aliyepimwa kiafya na kuonekana anayo afya nzuri na pia yule anayeonekana kuwa kiakili na maarifa anafaa. kwa maana hii ni kwamba anachagua 'cream' (wale bora) na kuwaacha 'wasiofaa' kwa maana nyingine. Na huyu mtoto anaenda kuwa Mmarekani, huku Malawi inabaki na wagonjwa na wasio na maarifa.
Ni kwanini Madona kama ana uchungu na Malawi asisaidie vituo vyote vya watoto yatima na kuwapatia huduma zote palepale Malawi. kwa jinsi hii atasaidia wamalawi wote na sio kwenda kuchukua wawili au watatu na kuacha maelfu ya watoto wakiwa hawana matumaini ya maisha bora!

No comments: