Friday, 6 March 2009

MJ na 'This is it'

Mfalme wa Pop Duniani, Michael Jackson, ametangangaza kuwa mwezi wa Saba mwaka huu atakuwa jijini London ktk ukumbi wa O2 Arena (zamani Millennium Dome) kwa ajili kuwatumbuiza wapenzi na mashabiki wake wa London (na Uingereza kwa ujumla) kwa mara ya mwisho.

Michael alitangaza mwenyewe jana 'live' majira ya saa 11 kwa saa za Uingereza na amesema atatoa burudani kwa kuimba nyimbo ambazo mashabiki wake wake wanazipenda.

Mimi ni mmoja wa mashabiki wa muziki wa Michael Jackson hasa nyimbo za 'The way you Make Me Feel', 'Earth Song', 'Man In the Mirror', 'Dirty Diana', 'Will You Be There' n.k.

No comments: