Monday, 2 March 2009

Mzee Madiba

Siku moja mwezi uliopita nilikuwa naangalia kipindi ktk tv stesheni ya bbc2 kuhusu maisha ya mzee Nelson Mandela. Kipindi kilikuwa kizuri sana hasa pale Mzee Madiba alipozungumzia historia yake kabla ya kwenda gerezani, akiwa gerezani na kutoka. Hata mke wake (Bi Graca) nae alitoa mpya pale alipomwomba mtalaka wake (Bi Winnie) apige picha na Mzee Madiba - Winnie akakaa kando ya Mzee na wakapiga picha ingawa Mzee hakutabasamu!

Baadae Mzee alipasua jipu pale aliposema kuwa alipokuwa gerezani kuna watu walimwambia kuwa Rais Mugabe (Z'bwe) hakutaka Mzee atoke gerezani. Mzee akasema kuwa alipokuwa gerezanai Rais Mugabe alikuwa mtu maarufu sana barani Afrika na hakutaka Mzee atoke kwa vile umaarufu wake ungepungua.

Hata hivyo Mzee Madiba alisema kuwa hayo ni maneno aliyokuwa anaambiwa na watu. kwa maana kwamba inawezekana ikawa kweli au sio kweli.

No comments: