Tuesday 31 March 2009

Tabia ya mtu - 2

Tue March 31, 2009
Zipo njia nyingi za kuweza kumuelewa au kumfahamu mtu kitabia au mwenendo wa kimaisha ikiwa haumuelewi au hamjafahamiana kwa kipindi kirefu au ndo mnakutana kwa mara ya kwanza.

Njia rahisi ambayo ninadhani inafaa kujua undani wa huyo mtu ni kupitia vyombo vya habari na pia kupitia njia ya maongezi ya kawaida au kwa simu.

Magazeti
Angalia anapenda kusoma magazeti gani (yapo magazeti ya aina na aina siasa, michezo na burudani n.k.). Pia ktk gazeti au magazeti anayopenda jaribu kuangalia anapenda kusoma kurasa gani -ukurasa wa mbele au nyuma (michezo) au za kati au hadithi, tamthiliya, makala n.k.

Redio na Televisheni
Siku hizi zipo stesheni nyingi sana za radio na TV. Je anasikiliza habari, miziki au michezo kwa upande wa radio. Kwenye Tv anapenda kuangalia nini zaidi.

Vitabu
Kama ni mpenzi wa vitabu anapendelea vitabu vya aina gani au fani gani; hadithi, sayansi, siasa, jamii, maisha n.k.

Hobby
Ni vitu gani anapendelea pale anapokuwa hana shughuli muhimu ya kufanya kutoka na kutembelea watu, kwenda kwenye kumbi za starehe au michezo, kufanya mazoezi n.k.

Maongezi ya kawaida
Ukiondoa salaam, kujuliana hali na kutambulishana, sehemu kubwa ya maongezi yanayofuata yanagusia au yanahusiana na nini.

Vitu au mali anazomiliki
Aina na thamani ya vitu anavyomiliki au mali yake, oanisha na jamii ya karibu nae kuona uwiano uliopo. Unaweza kupata kitu fulani cha ku-define mhusika.

Huwezi kukosa kumuelewa mtu kama utamtazama kwa tochi hii niliyodokeza. Hata busara na hekima za mtu huyo unaweza pia kuzipata kutumia tochi hiyo hiyo!

Kumbuka: haya ni maoni yangu binafsi, (kwa uzoefu wangu wa kula chumvi nyingi hapa duniani) na wala hayana uhusiano na mfano wowote hai.


(Maoni haya niliyatoa mara ya kwanza ktk mosonga.blogspot.com, Thursday, 11 September 2008. Labels: Autobiography)

No comments: