Wednesday, 3 June 2009

Vijana wadogo wasaidiwe

June III, MMIX
Natoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa watoto wote wanaoanza shule za msingi waruhusiwe kuendelea hadi kidato cha nne. Baada ya hapo, kwa wale ambao hawatapata nafasi kujiunga na kidato cha tano ama vyuo vingine (vya afya, kilimo, elimu n.k.) wapewe nafasi kujiunga na vyuo vya ufundi (VETA) moja kwa moja. Kwa maana hii karibu watoto wote watakaohitimu kidato cha nne watakuwa wamepata nafasi ya kujiandaa na maisha yao ya baadaye.

Hawa watoto watakapomaliza masomo/mafunzo yao popote pale watakapokuwa wameendelea (kielimu au ktk stadi mbalimbali kitaaluma), wataweza kujiajiri na hivyo kuwa walipa kodi wa miaka ijayo. Kinyume chake, kwa mtindo wa sasa, vijana kukaa mitaani kwa kisingizio cha kukosa ajira ni hatari kwa Taifa kiuchumi na kijamii kwa ujumla.

Vilevile natoa ushauri kuwa vijana wote watakaojiunga na mafunzo ktk vyuo vya VETA wadhaminiwe na serikali za mitaa kwa ushirikiano na serikali kuu. Kwa kweli serikali zetu zina uwezo wa kuwasaidia hawa watoto hawa ktk kujiandaa na maisha yao ya baadaye.

No comments: