Friday, 5 June 2009

Jamii na maisha

Mvuto kwa vijana wa jinsia nyingine
Kuwa na hamu ya ngono ni sehemu ya ujinsia. Kufanya ngono ni namna moja ya kuonyesha ujinsia , lakini ia unaweza kuonyesha ujinsia huu kwa kuongea, kushikana mikono, kupigana busu, kushikanashikana na kupapasana.

Mara nyingi madhumuni ya kufanya ngono ni kutaka kuzaa mtoto. Sababu nyingine za kufanya ngono ni kwa kujifurahisha, kuonyesha mapenzi na kuimarisha uhusiano wa kimapenzi. Jambo la msingi ni kuwa hapo utakapoamua wakati umefika wa kujihusisha na ngono umefika zingatia hiyo ngono iwe salama na kuwa wote yaani wewe na mwenzi wako mifurahie hiyo ngono.

Zamani au hata mila na desturi na desturi zetu zimetufanya tufikiri kwamba mwanamke pekee yake ndiye mwenye jukumu la kumfurahisha mume kwenye ngono bila mume kujali kama mpenzi wake naye ametoshelezwa.

Siku hizi angalau mambo yameeanza kubadilika na wanaume wengi wanatambua umuhimu wa kujali kumtosheleza mwenzi wake wakati wa kujamiiana. Tendo la ngono linakuwa nzuri pale wote wahusika watakapokuwa wamefanya kwa hiari, wametoshelezana na ngono hiyo ilikuwa salama ( hakuna mimba kama haikutakiwa, wala magonjwa ya zinaa au maambukizo ya UKIMWI)


chanzo: tovuti ya cheza salama (tanzania)

No comments: