Tuesday 9 June 2009

Bustani na maeneo ya kijani

Ktk nadharia ya mipango ya makazi (settlement planning) bustani na maeneo ya michezo zimegawanyika ktk madaraja kadhaa. Bustani sio kitu cha kukurupuka na kupachika tu popote utakapo!

1. Nyumba ya makazi (residential house) - kila nyumba inatakiwa itengewe eneo dogo la bustani. Kwa wenzetu wa UK karibu nyumba zote zina maeneo ya bustani kwa mbele au nyuma ya nyumba. Kwa sasa sina tarakimu za vipimo vya ukubwa wa bustani za kiwango hiki.

2. Kundi la nyumba (clusters) - kundi la nyumba 10 au zaidi linatakiwa kuwa na eneo lake kubwa kidogo la kuchezea watoto (play ground). Watoto au watu wa mtaa/mitaa jirani hukutana hapo kwa mapumziko ya muda mfupi ambapo pia watoto kucheza.

3. Bustani za kitongoji/kijiji (neighbourhood) - bustani hizi hukidhi mahitaji ya kitongoji au kijiji ambacho kina shule moja au mbili za msingi. bustani za kundi hili zina ukubwa zaidi ya zile za namba 1 na 2 hapo juu.

4. Bustani za 'wilaya' - hizi ni kwa ajili ya watu au eneo lenye vitongoji vingi (mathalani vitogoji zaidi ya 3) na lina maeneo ya maduka makubwa, ofisi za serikali/dola n.k. Bustani za daraja hili huwa ni kubwa zaidi ya zote hapo juu.

5. Maeneo yasiyowezekana kupangiliwa (cumbersome areas) - bustani za maeneo haya huwepo kutokana na kutokuwezekana kupangilia shughuli zozote, mfano za ujenzi wa nyumba za makazi ktk eneo husika na hivyo kutengwa kama eneo la kijani/bustani.

Kwa ujumla mji uliopangwa vizuri kwa kufuata kanuni za mipango miji huwa zina bustani za madaraja haya yote. Na inawezekana makundi tofauti ya bustani yakawa yanaungana ktk maeneo fulani (kutengeneza ukanda wa kijani) na hivyo kuwa mapito mazuri kwa waenda kwa miguu au baiskeli.

1 comment:

MOSONGA RAPHAEL said...

"Intelligence appears to be the thing that enables a man to get along without education. Education enables a man to get along without the use of his intelligence."

-Albert Edward Wiggin quotes,
quotes.liberty-tree.ca