Thursday 4 June 2009

R/Post sasa mara 2 kwa wiki

Juni IV, MMIX
Baada ya kuzorota kwa mauzo, wachapishaji wa gazeti la kila siku (jumatatu hadi Ijumaa) Reading Post wameanza utaratibu wa kuchapisha gazeti hilo kwa siku mbili tu kwa badala ya tano. Hii inatokana na hali ngumu kibiashara inayoyakabili magazeti mengi nchini Uingereza.
Mauzo ya magazeti mbalimbali yamekuwa yakishuka kila siku kutokana na hali ngumu ya uchumi kwa wasomaji na watangaza biashara kupitia magazeti hayo. Biashara na huduma mbalimbali za kijamii au kiuchumi zimedorora sana na hivyo kuathiri biashara ya magazeti.
Magazeti hutegemea sana matangazo ya biashara kimapato, na kipindi hiki ni kigumu kwa kila shirika au kampuni kibiashara. Hali inazidi kuwa mbaya hasa pale magazeti yanapopata ushindani kutoka kwa teknlojia ya utandawazi (internet). Biashara sasa hutangazwa mtandaoni ambapo huonwa na watu wengi na kwa haraka zaidi kutokana na ukweli kuwa wateja wengi sasa wanatumia kompyuta na internet ktk kupata habari na pia kwa kununua bidhaa bidhaa mbali mbali. Haya yote ni maendeleo ambayo yanasaidia ktk 'kuua' kizazi cha magazeti (print media).

Miaka minne iliyopita gazeti la Reading Post lilikuwa linauzwa kwa pensi 25 (25p). Hadi juma lililopita ktk toleo lake la mwisho la kila siku, nakala moja ilikuwa inauzwa 40p. Ktk toleo lake la kwanza jana nakala moja ilikuwa inauzwa kwa 20p na toleo la kesho Ijumaa litakalojulikana kama 'getreading' litauzwa kwa 40p na pia litasambazwa bure ktk nyumba zote za wakazi wa Reading.

Washindani wa Reading Post, Reading Chronicle nao wana wakati mgumu. Hivi karibuni walifanya mabadiliko makubwa kiutawala ktk kupunguza gharama. Walipunguza wafanyakazi na kuondoa/kuunganisha vitengo vingi. Aidha walibinafsisha baadhi ya huduma kwa wakandarasi ambao hulipwa kwa mkataba (badala ya kuwa wanfanyakazi wa kudumu). Reading Chronicle wana gazeti moja kubwa la kila wiki siku ya Alhamis ambalo huuzwa kwa 60p kwa nakala moja. Nao mauzo yao sio mazuri. Kadhalika wana magazeti ya bure ambayo husambazwa kwa kila nyumba Reading na vitongoji vyake (Winnersh, Wokingham, Lower Earley, Earley, Woodley, na sehemu za Sandhurst, Crowthorne, Slough, Windsor, Maidenhead n.k.) ktk siku za Jumatano. Magazeti yao ya bure hujulikana kama 'Midweek'.

No comments: