Tuesday 9 June 2009

'Gordon toa makaratasi'

Jana Waziri Mkuu wa UK Gordon Brown alifanya kikao na wabunge wa kutoka chama chake cha Labour ktk harakati za kutuliza vumbi la misukosuko ndani ya chama hasa baada ya Labour kufanya vibaya ktk chaguzi mbili (za serikali za mitaa na wabunge wa bunge la ulaya). Ktk chaguzi hizo Labour ilifanya vibaya sana na hata kujikuta ikishika nafasi ya tatu chini ya 'makonsevativu' na chama kidogo cha 'ukip'.
Pia matatizo ndani ya Labour yalisababishwa na wabunge kudai malipo ya masurufu (expenses) hata ambayo hawakustahili kulipiwa na serikali! Ktk sakata hili baadhi ya mawaziri na manaibu kadhaa ilibidi waachie ngazi na wabunge kadhaa nao kutangaza kuachia ngazi ktk uchaguzi ujao (hawatagombea tena)!

Ktk kikao cha jana jioni, wabunge walimwambia WM Brown 'asafishe nyumba' la sivyo ataachishwa kazi!

Miongoni mwa masharti aliyopewa ili waendelee kumuunga mkono ni kufuta sera yake ya kubinafsisha (partly privatisation) shirika la posta na Royal Mail. Wabunge wengi hawaungi mkono ubinafsishaji wa Royal Mail. Pia WM ameambiwa alinde ajira za wafanyakazi ambao inaelekea wengi wao wako ktk hatihati ya kupoteza ajira zao ktk makampuni na mashirika kadhaa. Kuna baadhi ya sera mpya za WM Brown ambazo hazikuwafurahisha wabunge na wananchi kwa ujumla ambao ndio wapiga kura. Kwa mfano kuondoa kiwango cha kodi cha watu wa kipato cha chini cha asilimia 10 na kukifanya kuwa asilimia 20 kwa wote (flat rate) - uamuzi huu umewaumiza watu wengi sana wa kipato cha kawaida. Hata matajiri nao hawakufurahishwa na uamuzi wa serikali wa kuongeza kiwango cha kodi kutoka asilimia 40 hadi 50.

Suala la uhamiaji nalo bado linaisumbuia serikali na limechangia pia kushindwa vibaya kwa serikali ktk uchaguzi. Hata hivyo baadhi ya wabunge wamemtaka WM Brown awahalalishe wanaoishi na kufanya kazi UK bila vibali ili waweze kuwa raia kamili na kushiriki kikamilifu ktk kuijenga nchi yao. Wabunge hao wamekasirishwa na uamuzi wa serikali kuendelea kutowatambua watu wanaoishi nchini bila vibali. Mbunge mmoja alisisitiza mbele ya mtangazaji wa tv nje ya ukumbi wa bunge kwa kusema 'hawa watu wapo nchini, na pia wanafanya kazi kichini chini, ni kwanini wasipewe vibali (makaratasi)?

No comments: