Thursday 16 April 2009

Sera na mfumo wa Afya TZ

Leo nimepita Broad Street, mjini Reading na kukuta wafanyakazi kutoka NHS wakifanya kampeni ya kuitangaza NHS na kuulizia wananchi wanaonaje huduma za NHS. Kampeni hii inaitwa 'Your health, your way, your choice. (It's your choice)'

Wakazi wa Uingereza wanapewa nafasi kutoa maoni yao juu ya kazi nzuri au mbaya na udhaifu iliopo NHS. Na kwa upande wao, NHS wanawasiliza wananchi ili kuboresha huduma zao. Hii ni kampeni ya nchi nzima.

Majuzi pia kulikuwa na kampeni ya NHS kuhusu madhara uvutaji (smokefree campaign) sigara kiafya na kiuchumi. Kwa kuzingatia hivi sasa hali ya maisha kiuchumi ni ngumu kwa wakazi wa UK NHS ilitumia nafasi hiyo kuwaelimisha wananchi hasa wavuta sigara jinsi wanavyopoteza fedha zao kwa kununua sigara. Kwa hesabu za NHS ilibainika kuwa mvutaji wa kawaida hupoteza Paundi 176 kwa mwezi (£2,111 kwa mwezi)kutokana na kuvuta sigara (kwa wavutao pakti moja ya sigara kwa siku)!

Zipo kampeni nyingi tu zinazoendeshwa na NHS, na ni endelevu.

Sera kama hizi zinafaa kuigwa nyumbani kwetu. Ni kiasi cha kuamua sasa na kubadilisha mambo kwa manufaa ya wananchi. Hii ni kazi au wajibu wa wanasiasa kulitilia mkazo jambo hili. Mtaji wa fedha upo. Kuna 'vijisenti' vingi tu vya serikali vinaishia mifukoni mwa wachache. Nidhamu ktk kazi inaweza kuvielekeza 'vijisenti' hivi ktk maeneo nyeti kwa ajili ya maslahi ya wananchi, afya ikiwa mojawapo.

No comments: