Friday 24 April 2009

HQ wilaya ya Rorya: Rais kakosea?

Jana nimesoma gazeti kuwa Rasi Jakaya Kikwete amekata mzizi wa fitina kwa kuchagua kijiji fulani kuwa makao makuu ya wilaya ya Rorya.

Ktk enzi hizi za demokrasia sio vizuri kwa mkuu wa nchi kuchagulia wananchi ni wapi pawe makao makuu yao. Serikali ilifanya uamuzi mzuri wa kuunda wilaya mpya ya Rorya, ila sidhani kuwa ni busara tena kuwachagulia wana-Rorya makao yao makuu.

Kama kulikuwepo mgogoro kuhusu ni wapi yawe makao makuu, basi ingeundwa tume huru ya wataalamu (tawala za mikoa) ili ichunguze na kuainisha eneo muafaka kwa ajili ya makao makuu ya wilaya halafu tume ingetoa mapendekezo kwa waziri mkuu ambaye wizara ya tawala za mikoa iko chini yake.

Ni kwa kuzingatia mapendekezo ya tume pekee ndipo serikali ingetoa tamko husika lakini sio kwa Rais mwenyewe kuingilia. Kuna mabo mengi sana nchini ambayo hayajapatiwa ufumbuzi miaka nenda rudi, mbona Rais hajayatolea tamko?

Inawezekana kabisa hapo alipopendekeza Rais ndipo panafaa, ila tatizo ni kuwa ameingilia. Ni vizuri nchi iendeshwe kwa misingi hai ya demokrasia na utawala wa sheria. Siamini kuwa hili tatizo liliwashinda madiwani, wataalamu -tawala za mikoa na waziri husika hadi ofisi ya waziri mkuu.

Nina imani kama kuna wana-Rorya ambao hawakufurahia agizo la Rais wanaweza kutumia haki yao kisheria na kikatiba kwenda mahakamani kudai kupitiwa upya utaratibu uliotumika kuamua jina la makao makuu.

Ipo miji kama Ochuna, Kowaki na Shirati ambayo imeshajengeka na ni rahisi kuogezea ofisi za makao makuu ya wilaya. Kijiji alichochagua Rais hakina huduma nyingi, na itakuwa gharama sana kukinyayua hadi kufikia hadhi ya makao makuu. Tusisahau ya Dodoma, tangu pawe makao makuu ya nchi mwaka 1973 hadi leo wazito wanaishi Dar (nyumba walijengewa lakini hawataki kuhamia!), wanaenda na tu kuhudhuria vikao vya chama au bunge na kurudi Dar, sembuse kule Rorya!

No comments: