Tuesday, 21 April 2009

Madawa ya kukuza miili (misuli) yanaua

Tuesday, 21/04/2009
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia jana asubuhi hospitalini alipokuwa amelazwa kutokana na 'side effects' za madawa ya kutunisha misuli (body building) aina ya 'steroids'.
Kwa mujibu wa gazeti la leo la Daily Mirror, wazazi wa kijana huyo wamesema kuwa kifo cha mtoto wao kilisababishwa na kuvimba ubongo na hatimae kupoteza fahamu (ubongo ulikufa) kutokana na kuzidiwa na madawa hayo ambayo aliyanunua kienyeji. Kijana huyo alikunywa dawa hizo ili ajenge misuli na hatimae afaulu usaili wa kujiunga na jeshi nchini Uingereza.
Watu waliomuuzia dawa hizo marehemu wamekamatwa na polisi na kusailiwa na kisha kuachiwa kwa dhamana.
Wazazi wa marehemu wameomba kuwa kifo cha mwanao kiwe funzo kwa wengine wenye tabia kama hiyo - na wamewataka vijana kuachana na madawa hayo ili yasije yakawakuta yaliyomkuta kijana wao mpendwa!

No comments: