Saturday, 3 January 2009

Wafanyakazi na muda wa kazi

Muda maalumu uliopangwa kwa wafanyakazi wa serikali huwa ni saa 8 kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kwa jumamosi huwa ni nusu siku.

Mara nyingi uatona wafanyakazi nchini tanzania wanaendelea kuwepo maofisini hata baada ya muda wa kazi kupita hadi saa za usiku. Siku za Jumamosi na Jumapili pia huwa wanaenda maofisini.

Nimebahatika kukaa nje ya bara la Afrika na nimeona jinsi wenzetu wanavyo heshimu muda wa kuingia kazini na wa kutoka kazini. Na pia wanaheshimu sana siku wanazokuwa off, kwasababu ni muda adimu kwa ajili ya mambo yao binafsi na pia kujumuika na familia au mambo yahusuyo familia.

Familia zinahitaji muda na ndio maana serikali za ulaya hutoa likizo kwa wazazi wote (mama na baba) ili walee watoto mama anapojifungua. Muda wa kazi ni wa kazi, muda wa off ni off. Sio vibaya waafrika tukiiga hili kwa manufaa yetu na familia zinazotuhusu. Tuachane ni porojo za 'niko bize!'

No comments: