Friday 30 January 2009

'Uzawa' waingia Uingereza!

Umeshasikia kauli mbiu ya Waingereza siku hizi? Baada ya hali ya uchumi kuwa mbaya, wazawa wa UK wamekuja na mpya! Wanadai kuwa nafasi zote za kazi nchini kwao ni kwa ajili yao tu - yaani wazawa wa UK!!

Leo waliandamana mahala fulani kupinga kampuni moja iliyoko UK kuajiri wafanyakazi toka Italia na Ureno, wakiwa na mabango yasemayo:
'UK jobs for UK workers'!

Tena ni afadhali watu wanaotoka maeneo ya Jumuia ya Ulaya, maana sheria za EU zinawalinda kufanya kazi popote ndani ya EU. Hali ni mbaya kwa wenzangu mie wanaotoka nje ya eneo la EU (kwa mfano Afrika, Asia na Amerika Kusini). Miaka ijayo watu wasio wakazi wa EU watapata wakati mgumu sana nchini UK kwani sheria* zinatungwa ili kuwazuia kuja kufanya kazi UK na hata kama watakuja kwa ajili ya kusoma, hawataweza kupata ruhusa ya kuajiriwa/kufanya kazi maana vitambulisho vya wasio raia vimeshaanza kutumika kwa hiyo itakuwa vigumu kupata ajira ya kujikimu kimaisha!

Uzalendo umeanza kuwashinda Waingereza na sasa wameshikilia sera za Uzawa.

Je, wa-kuja tutafika kweli?
.............................

*Australian Points Based System (PBS).

No comments: