Tuesday, 27 January 2009

Maisha juu

Kuna bidhaa mimi hupenda kununua kwa ajili ya matumizi muhimu hasa chakula na vimekuwa vikipanda bei kwa kasi kubwa.
Jam 450g (mixed fruit) ilikuwa 30pence (£0.30) mwaka mmoja uliopita sasa ni 38p
jam (450g conserv.) ilikuwa 79p mwaka mmoja uliopita sasa ni £1.09
mkate (farmhouse) 56p (85p)
maziwa (lita 2.72 sawa na 2 Pints) 99p (£1.49)
vitunguu 29p (69p)
Peanuts smooth 450g, 79p (95p)
ndizi mbivu 1kg., 45p-66p (85p-97p)

Bado hujagusa unga, nyama, mboga za majani, matunda, juisi, maji ya chupa, maharage n.k. ambavyo vyote vimepanda.

Bei hizi ni za duka la Lidl. Hata maduka makubwa kama tesco, sainsburys, morrison, asda nako bei za vitu zimepanda kweli. Kwa maduka madogo ya mitaani (convenience stores) bei zake ni kubwa zaidi!

Zamani bei za vyakula UK zilikuwa ni ndogo kiasi kwamba karibu kila mtu alikuwa anamudu. Siku hizi mambo yamebadilika.

Nauli za mabasi ya abiria nazo zimepaa. Miaka 3 iliyopita nauli ya kwenda (one way) ilikuwa £1.00, (£1.30 tiketi ya mzunguko siku nzima) leo hii ni £1.65 one way na £3.20 mzunguko siku nzima.

Na tayari imeshatangazwa rasmi kuwa UK iko ktk matatizo makubwa kiuchumi ambapo wataalamu wa mambo ya uchumi wanatabiri mambo yataendelea kuwa magumu hadi mwaka 2011 mwishoni.

Huu ni mwanzo wa safari ndefu ndani ya 'economic recession' na wataalamu hao wanaomba hii 'recession' isijegeuka kuwa 'depression'!!

No comments: