Friday 4 April 2008

Kina dada!

Utafiti umeonyesha kuwa kina dada wengi huwa wanafurahia pale wanaume wanapowapulizia mluzi kama kuonyesha ishara ya kuwapongeza waliopendeza njiani.

Madada wengi wenasema kuwa kupigiwa mluzi au sauti fulani kutoka kwa wanaume ni ishara kuwa mdada amependeza, na madada wengine hujiuliza 'kulikoni' pale wanaume wanapokuwa kimya mitaani! Wengine wanasema kuwa miluzi inawaopa ujiko na kujiona kuwa 'wametoka' poa kimavazi na kiurembo.

Habari hizi ni kwa mujibu wa matangazo ya Tv kupitia kituo cha 'bbc one' ktk kipindi cha 'breakfast' leo asubuhi.

Wadada karibu wote waliohojiwa walisema hakuna tatizo kwa wanaume kuwashangilia!

Kwa kweli ni kawaida hata kwetu Afrika, vijana wa kiume kuonyesha ishara fulani ya kisauti (wakati mwingine 'busu' la kiaina), pale wanapopendezwa na urembo wa dada au madada fulani njiani. Hii ni kawaida.

*Samahani:
Sikutumia neno kina mama.
Kwa kuheshimu kuwa wengi wao ni wake wa watu; na wengine wanaweza kujisikia vibaya. Hivyo nisingependa kuwakwaza.
Lakini ukweli ni kwamba akina mama nao wanapendeza! Sio vibaya kuwapongeza!

No comments: