Tuesday 22 April 2008

Elimu, madaraka na uaminifu!

Mara nyingi mimi husikia watu wakiulizia watu wenye wadhifa au madaraka fulani kuwa wana elimu gani. Wingi wa miaka masomoni huashiria mtu husika kukubalika ktk cheo alichonacho.

Sina tatizo na hilo.

Jamii yetu inahitaji walioenda shule ili iwakomboe wao na vizazi vyao. Pata elimu, rudisha 'kitu' kwa jamii kupitia utumishi wako au ujuzi wako - ndivyo inavyotakiwa.

Lakini kuna baadhi ya walienda shule (wasomi) tena wamebobea ktk nyanja walizosomea wamekuwa wakichafua umuhimu wa elimu.

Sina haja ya kwenda mbali.

Kwani walioweka mikataba ya feki yenye kuumiza wananchi wameenda shule au ni vihiyo?

Jamani kihiyo anaweza kupata wadhifa wa juu wizarani hadi kusaini mukataba ya kimataifa? Haiwezekani. Kwa hiyo wahusika ni wasomi tena waliobobea. Hilo halina ubishi.

Misamaha ya kodi kwa wawekezaji kwa miaka mitano, kisha wanatimua au wanabadilisha majina na wanapewa miaka mitano tena ya msamaha wa kodi -yaani wanarithishana kutoka mzazi hadi mjukuu kwa miaka mitano mitano huku sisi waTZ hatuambulii chochote.

Mikataba ya madini isiyo na uwiano sawa kati ya mwananchi na mwekezaji. Inamlinda zaidi mwekezaji huku mwananchi akibaki mtupu na mashimo matupu ya migodi.

Mikataba ya rada, IPTL, Richmond na Dowans Ltd. Hadi uchotaji wa hela Benki Kuu (EPA) n.k.

Usisahau, ununuaji jengo 'hewa' la ubalozi Italia uliofanywa na balozi tena profesa!!

Kashfa zote hizi zinafanywa na wasomi walioenda shule!

Watoto wetu wanajifunza nini juu ya ubadhirifu wa kiwango hiki. Mimi naona kinakuja kizazi cha 'soma, iba, tajirika'!

No comments: