Tuesday 6 November 2007

Matokeo: Waliogombea NEC-CCM, 2007

Leo napitia orodha ya walioomba ujumbe wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa ili kuona kama wamefanikiwa. Orodha ya wagombea ilitolewa 03/8/2007. Tayari Mkutano Mkuu wa kawaida wa CCM umeshafanyika na orodha ya washindi imepatikana!
Na Mosonga

03 Aug 2007
Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana kilitoa hadharani majina ya wanachama wake watakaogombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia makundi mbalimbali.

A) Tanzania Bara Viti 20:

Waziri Mkuu,
Bw. Edward Lowassa - AMESHINDA

Bi. Shy-Rose Bhanji -AMEKOSA

Waziri wa Ulinzi,
Profesa Juma Kapuya - AMESHINDA

Naibu Waziri wa Miundombinu
Dk. Milton Makongoro Mahanga -AMESHINDA

Katibu Mkuu wa CCM,
Bw. Yussuf Makamba -AMESHINDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Bernard Membe -AMESHINDA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Bw. William Ngeleje,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Siasa)
Bw. Kingunge Ngombale Mwiru - AMESHINDA

Waziri Mkuu Mstaafu
Bw. Frederick Sumaye -AMESHINDA

Bw. Wilson Masilingi,
Bw. Filbert Bayi,
Bw. Abrahaman Kinana -AMESHINDA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Bw. William Lukuvi

Bw. Jaka Mwambi -AMESHINDA

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki
Bw. Deodarus Kamala -

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na ushirika
Bw. David Mathayo -

Bw. Aggrey Mwanri -AMESHINDA
Bw. Isidore Shirima -
Bw. Enock Chambili -
Bw. Christopher Gachuma -AMESHINDA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Profesa David Mwakyusa -AMESHINDA

Profesa Samwel Wangwe -AMESHINDA

Waziri wa Miundombinu
Bw. Andrew Chenge -AMESHINDA

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
Bw. Capt. John Chiligati -AMESHINDA

Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi -
Kapteni John Komba -AMESHINDA

Bw. Novatus Makunga -
Bw. Tarimba Abbas -
Bw. Lucas Kisasa -AMEKOSA
Bw. Job Ndugai -
Bw. George Simba Chawene -
Bw. Abdul Sapi -
Bw. Uhahula -
Bw. David Holela -

Waziri wa Kilimo na Ushirika,
Bw. Stephen Wassira -AMESHINDA

Bw. Emmanuel Mwambulukutu,
Bw. Amos Makalla -AMESHINDA
Bw. Jackson Msomi (Msome?) -AMESHINDA
Dr. James Msekela,
Bw. Mohamed Mkumba,
Prof Idris Mtulia,
Bw. Pascal Mabiti,
Bw. Said Fundikira,
Bw. Abeid Mwinyimusa,
Bw. Charles Kagonji na
Dk. Ibrahim Msengi.

B) Zanzibar:

Dk. Ali Mohamed Shein -AMESHINDA

Waziri Kiongozi,
Bw. Shamsi Vuai Nahodha -AMESHINDA
Dk. Hussein Mwinyi -AMESHINDA
Dk. Gharib Bilal -AMESHINDA
Bw. Mohamed Seif Khatibu -AMESHINDA
Bi. Samia Suluh Hassan -AMESHINDA
Bi. Kidawa Hamid Saleh -AMESHINDA
Bw. Salim Msabah -AMESHINDA
Bi. Khajida Aboud -AMESHINDA
Bw. Mansour Yusuf -AMESHINDA
Bw. Mohamed Nassor Moyo -AMESHINDA
Bw. Makame Mnyae -AMESHINDA
Bi. Moudeleine Castico -AMESHINDA
Bw. Twaiba Kisaso -AMESHINDA
Bi. Ishao Abdallah Ussu -AMESHINDA
Bw. Vuai Ali Vuai -AMESHINDA
Bw. Omary Yusuf Mzee -AMESHINDA
Bw. Adam Mwakanjuki -AMESHINDA

C) Wanawake Zanzibar:
Bi. Mwajuma Abdallah Majid -AMESHINDA
Bi. Fatma Said Ali -AMESHINDA
Bi. Fatma Aloo -AMESHINDA
Bi. Amina Idi Mabrouk -AMESHINDA
Bi. Catherine Nao -AMESHINDA
Bi. Asha Abdallah Juma -AMESHINDA
Bi. Asha Bakari Makame -AMESHINDA

Baadhi ya wanaogombea ujumbe wa NEC kupitia Vijana Bara ni
Bi. Zainabu Kawawa -AMEPATA
Bw. Nape Nnaunye -AMEPATA
Bw. Deogratias Ndejembi -
Bw. Paul Kirigiri -
Bw. Maghembe Maghembe -
Bi. Violet Mzindakaya -AMESHINDA
Bi. Lucy Mayenga -AMEPATA
(majina yafuatayo sikuyaona August 2007)
Bi. Jerry Slaa -AMESHINDA
Bw. Salim M. Ali -AMESHINDA
Bw. Suleiman Mchabi -AMESHINDA
Bw. Beno Malisa -AMSHINDA
Bw. Edwin Sannda -AMESHIDA (hongera 'mate' - uclas!)

Vijana (UVCCM) Zanzibar:
Bi. Hawa Sukwa Saidi -AMESHINDA
Bw. Hamad Yusuf -AMESHINDA
Bi. Adika Vuai -AMESHINDA
Marco Charles Bundara -AMESHINDA
Ashura Abdallah Ismail -AMESHINDA
Suleiman M. Haji -AMESHINDA

Ujumbe NEC Wazazi Tanzania Bara baadhi ya majina mashuhuri ni yafuatayo:
Bw. Enock Kalumuna,
Bw. Salim Tambalizeni,
Bw. Richard Hizza Tambwe - AMEKOSA
Bw. Mustapha Yakub,
Bw. Mussa Hassan Zungu -AMESHINDA
Bw. Ruth Msafiri, .....(bwana au bi?)
Bw. Thomas Ngawaiya - AMEKOSA
Bw. Henry Shekifu,
Bw. Richarch Nyaulawa -AMESHINDA
Bw. Danhi Makanga - AMEKOSA
Bw. Dickels Shindika,
Dr. Zainabu Gama -AMESHINDA
Bw. Adam Kighoma Malima -AMESHINDA
Bw. Stella Manyanya -AMESHINDA
Bw. Athumani Mfutakamba -
(hili jina sikuliona Augosti 2007)
Bw. Mohamed Nondo -AMESHINDA

Wazazi Zanzibar:
Dogo Mabrouk -AMESHINDA
Hassan Rajab Khatibu -AMESHINDA
Fatma A. Haji -AMESHINDA
Mtumwa Pea -AMESHINDA

D) Wanawake (UWT) Bara:
Bi. Halima Mamuya -AMEKOSA
Bi. Sifa Swai -
Bi. Asha Baraka -AMEPATA
Bi. Khadija Kopa -AMEPATA
Bi. Jacqueline Liana -AMEKOSA
Bi. Anne Makinda -AMEPATA
Bi. Jane Mihanji -AMEKOSA
Bi. Fatuma Adam Mkwawa,
Bi. Rita Mlaki -AMEKOSA
Bi. Sofia Simba -AMEPATA
Bi. Margaret Sitta -AMEPATA
Bi. Kate Kamba -AMEPATA
Bi. Shamsa Mwangunga -AMEPATA
Bi. Anne Kilango Malecela -AMEPATA
Bi. Salome Mbatia -AMEFARIKI DUNIA
Bi. Zakia Meghji -AMEPATA
Dr. Rehema Nchimbi -AMEPATA
Bi. Halima Kihemba -AMEKOSA
Bi. Margaret Mkanga,
Bi. Lydia Boma,
Bi. Esther Nyawazwa,
Bi. Zainab Vullu ,
Bi. Esha Stima -AMEKOSA
Bi. Diana Chilolo -AMEPATA
Bi. Tatu Ntimizi -AMEKOSA
Dr. Aisha Kigoda -AMEPATA
Bi. Mwantumu Mahiza -
Bi. Beatrice Shelukindo -AMEKOSA
Bi. Pili Chana -AMEPATA (nimeliona leo, awali sikuliona hili jina!!)

Taarifa hiyo inaonyesha kwamba wana-CCM
60 wameteuliwa kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC Taifa kwa upande wa Tanzania Visiwani,
18 kupitia UVCCM,
12 kupitia Wazazi na
21 kupitia UWT.

Wana-CCM kadhaa wameamua kutangaza rasmi kung’atuka katika uongozi wa chama. Waliochukua hatua hiyo ni:-
Dk. Chrisant Mzindakaya,
Bi. Maria Watondoha,
Balozi Isaack Sepetu,
Bw. Daniel Ole Njoolay,
Bw. Charles Keenja,
Profesa Philemon Sarungi,
Bw. Stephen Mashishanga,
Bw. Paul Kimiti,
Bi. Asha Makwega na
Bi. Shamim Khan.
Bw. Pancras Ndejembi (M/Kiti mkoa, Dodoma).


Kamati ya usimamizi wa uchaguzi CCM:
1. Spika Sitta -M/Kiti
2. Makamu wake Anna Makinda (?)
3. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,
Bw. Pandu Ameir Kificho,
4. Dk. Maua Daftari,
5. Dk. Mary Nagu,
6. Dk. Batilda Burian,
7. Bw. Rostam Azizi na
8. Bw. Emmanuel Nchimbi.

Halmashauri Kuu inakutana leo, 06/11/2007, kuteua Kamati Kuu ya CCM na secterarieti na jina la Katibu Mkuu wa CCM.


HABARI ZAIDI (KUTOKA KWA ISSAMICHUZI BLOG)
MANAIBU mawaziri watano, wakuu wa wilaya na viongozikadhaa wa zamani wa chama na serikali na wanasiasawatatu wa upinzani waliohamia Chama Cha Mapinduzi(CCM) hivi karibuni, ni miongoni mwa walioshindwakatika uchaguzi wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifaya chama hicho (NEC).

Wakati wanasiasa hao wakishindwa kuingia ndani yaNEC, watendaji wakuu wa chama hicho akiwamo KatibuMkuu, Yussuf Makamba na mawaziri kadhaa wakiongozwa naWaziri Mkuu Edward Lowassa, walishinda uchaguzi huouliofanyika juzi wakati wa Mkutano Mkuu wa Taifa waNane wa CCM uliomalizika jana alasiri kwenye Ukumbi wa Kizota hapa.

Manaibu mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nnewalioshindwa ni Rita Mlaki (Ardhi, Nyumba na Maendeleoya Makazi) na Mwantumu Mahiza (Elimu na Mafunzo yaUfundi) walioshindwa kwa kundi la viti 13 WanawakeBara.

Wengine ni Dk. Diodorus Kamala (Ushirikiano waAfrika Mashariki), Dk. David Mathayo (Chakula,Ushirikana Masoko) na William Ngeleja (Nishati na Madini)walioshindwa kupitia kundi la viti 20 Tanzania Bara.

Katika uchaguzi huo, walioanguka wengine waliopitia katika kundi la Wanawake Bara ni aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Tatu Ntimizi, Katibu Mkuu wa zamani wa UWT, Halima Mamuya, wakuu wa wilaya;Halima Kihemba, Chiku Galawa, Fatma Kimario, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Mrisho, wabunge; EstherNyawazwa, Zainab Vullu, Margaret Mkanga, BeatriceShelukindo na wanahabari Jacqueline Liana na Jane Mihanji, wote wa Uhuru/Mzalendo.

Walioshinda na kura zao katika mabano ni MargaretSitta (1,780), Zakia Meghji (1,207), Pindi Chana(1,203), Anne Makinda (1,146), Diana Chilolo (1,105),Dk. Aisha Kigoda (1,060), Anne Kilango-Malecela (983),Dk. Rehema Nchimbi (887), Shamsa Mwangunga (850),Khadija Kopa (842), Asha Baraka (766), Kate Kamba(706) na Sophia Simba (689).

Katika kundi la Tanzania Bara, mbali na akina Dk.Mathayo, Dk. Kamala na Ngeleja, wengine waliotupwa nje ni wakuu wa mikoa; Dk. James Msekela, Isdori Shirima, Abeid Mwinyimsa, wakuu wa wilaya; Pascal Mabiti, Frank Uhaula, David Holela, Dk. Ibrahim Msengi, waandishi wa habari Lucas Kisasa, Shy-RoseBhanji na Novatus Makunga.

Wengine ni Balozi Emmanuel Mwambulukutu, mawaziri wa zamani Wilson Masilingi, Hassan Ngwilizi, Mwenyekiti wa zamani wa Mkoa wa Mara, Enock Chambiri, Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi na wabunge; Profesa Idrisa Mtulia na Job Ndugai na mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Salim Hamis Salim ‘Chicago’.

Katika kundi hilo la ‘kifo’, waliopenya ni Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliyeongoza kwa kura 1,681, Andrew Chenge (1,530), Yussuf Makamba (1,510), Bernard Membe (1,281), Jaka Mwambi (1,239), Profesa Juma Kapuya (1,216), Abdulrahman Kinana (1,204),Christopher Gachuma (1,181), Stephen Wassira (1,107),Aggrey Mwanri (1,068), Milton Mahanga (1,067),Frederick Sumaye (1,065).

Pia wamo John Komba (1,056), Kingunge Ngombale-Mwiru(1,023), John Chiligati (910), Amos Makalla (871),Profesa Samuel Wangwe (817), Profesa David Mwakyusa(754) na Jackson Msome (747).

Wanasiasa waliojiunga na CCM kutoka vyama vyaupinzani; Richard Tambwe Hizza na Thomas Ngawaiya walikwama baada ya kushindwa katika Kundi la Wazazi Bara, huku kiongozi mwingine wa zamani wa upinzani,Salum Msabah Mbarouk akishinda kwa upande wa viti 20 kundi la Tanzania Visiwani.

Mbali na Tambwe na Ngawaiya, wengine walioshindwa kwa Wazazi ni mshairi maarufu Salim Tambalizeni, wakuu wawilaya; Danhi Makanga, Athuman Mfutakamba, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, mbunge Ruth Msafiri(Muleba Kaskazini).

Walioshinda ni Stella Manyanya (948), Zainab Gama(818), Mussa Azzan Zungu (730), Adam Kighoma Malima(698), Mohammed Nondo (679) na Richard Nyaulawa (669).

Kwa upande wa Zanzibar kundi hilo la Wazazi, washindini Dogo Iddi Mbarouk, Fatma Abeid Haji, Mtumwa YussufPeya na Hassa Rajab Khatib.

Walioshinda kwa upande wa Umoja wa Vijana Kundi la Bara ni Zainab Kawawa (1,390), Violet Mzindakaya Mpogolo (1,165), Nape Nnauye (1,056), Jerry Silaa(994), Sarah Ally (935), Beno Malisa (857), EdwinSanda (804) na Lucy Mayenga (770).

Miongoni mwa walioshindwa katika kundi hilo ni mgombea Penias Kaindoa ambaye wakati akiomba kura,aliwasihi wajumbe wamnusuru ili asiwe mkimbizi kwenye nchi yake, akitokea katika Jimbo la Bukoba Mjini lenye upinzani mkali na Chama cha Wananchi (CUF), akidai akirudi bila kuchaguliwa, atakuwa katika wakati mgumu.

Washindi kwa upande wa Vijana Zanzibar ni Hawa SukwaSaidi (930), Hamad Masauni Yussuf (894), Adila HilalVuai (886), Michael Charles Bundala (845), AshuraAbdallah Ismail (808) na Suleiman Muhsin Haji (771).

Washindi kwa upande wa Tanzania Visiwani ni Dk. AliMohamed Shein (1,663), Shamsi Vuai Nahodha (1,525), Dk. Hussein Ali Mwinyi (1,496), Dk. Mohammed GharibBilal (1,366), Saleh Ramadhan Ferouz (1,352), Muhammed Seif Khatib (1,346), Samia Suluhu Hassan (1,281),Kidawa Hamid Saleh (1,212), Msabah (1,151), Khadija Hassan Aboud (1,076), Mansour Yussuf Himid (1,073),Omar Yussuf Mzee (1,022), Balozi Seif Ali Iddi (997),Mohamed Hassan Nassoro Moyo (959), Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (958), Maudline Cyrus Castico (950),Vuai Ali Vuai (943), Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki(936), Thuwayban Edington Kissasi (860) na Dk. Ishau Abdula Khamis (840).

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa upande wa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa alipata kura za Ndiyo 1,879, na kura tano za Hapana, kati ya kura halali 1,887, huku kura moja ikiharibika na ushindi wake ni sawa na asilimia 99.78.

Sitta alisema kwa upande wa Makamu Mwenyekiti TanzaniaZanzibar, Rais Amani Abeid Karume alishinda kwa kupatakura 1,886 za Ndiyo, kati ya kura 1,887. Kura moja ilimkataa na ushindi wake ni sawa na asilimia 99.94.

Rais Jakaya Kikwete ambaye tangu Juni 25, mwaka jana alikabidhiwa mikoba ya uenyekiti wa CCM na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, jana alikabidhiwa rasmi kipindi chake cha kwanza kwa kuchaguliwa kwa kura za Ndiyo 1,887, kati ya kura halali 1,892, kura tanozi kimkataa na hivyo ushindi wake ni sawa na asilimia 99.73.

Mwenyekiti huyo mpya wa CCM alitangaza kuwa leo Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho itakutana kwamara ya kwanza na kisha kuteua Kamati Kuu na kuundwakwa Sekretarieti mpya itakayoiongoza CCM kwa miakamitano hadi mwaka 2012.

Kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Nane wa CCMjana kulihitimisha mchakato wa uchaguzi ndani ya chamahicho ulioanza Januari mwaka huu kuanzia ngazi ya Shina.

No comments: