Monday 12 November 2007

Nguvu za Kiume

Jamani, jamani, jamani, kuna jirani yangu kafa hivi majuzi. Alikuwa ni baba wa makamu, mmarekani mweusi. Alikuwa mcheshi na ilikuwa kila tukionana lazima tusalimiane. Mara ananinunulia kahawa halafu tunakaa namsimulia kuhusu Afrika. Yule baba, alionekana mzima na mwenye afya fiti kabisa. Nilibakia kushangaa kusikia kafa na si kwa ajali. Mke wake alifariki mwaka juzi, lakini miezi ya karibuni alikuwa anaonekana mwenye furaha kwa vile alipata mpenzi, dada mwenye miaka 25 hivi.

Story niliyoskia ni hivi:
Kumbe jamaa alikuwa na matatizo ya moyo. Alifia kitandani akiwa kwenye shughuli ya kufanya tendo la ndoa na mpenzi wake. Tena wanasema alifariki mara alipofikia kilele cha tendo. Navyosikia ilikuwa ni ‘massive heart attack’. Kama ni massive bila shaka na utamu wa shughuli hakujua kuwa yuko hatarini.

Nasikia huyo mpenzi wake alipiga sana makelele majirani walipigia simu polisi 911 kwa vile walidhania wameingiliwa na majambazi. Wanasema baba wa watu kamwangukia yule dada na kafa macho wazi.Lakini bado nilikuwa nashangaa maana kama nilivyosema awali, jamaa alionekana kuwa na afya. Kumbe jamaa alikuwa mtumizi wa Viagra, yaani vile vidonge vya kuongeza uume, na kumpa mwanaume uweza wa kufanya tendo la ndoa.

Ndugu zake wanalalamika kweli, maana hakuzipata kwa prescription ya daktari, alizaiagiza kwenye mtandao (internet). Kwa kumwangalia alivyofiti nisingefikiria kuwa ana matatizo ya nguvu za kiume.

Kumbe mtazame mtu, matatizo yake anayajua mwenyewe na daktari wake.

Nikawa najiuliza kama jamaa alijua ana matatizo ya moyo, kwa nini alitumia Viagra. Maana hata tangaza kwenye TV na magazeti wanaonyo kuwa kabla ya kutumia. Halafu pia wanaonya kuwa mwanaume anaweza kupofuka kama anatumia. Lakini wanaume bado wanazitumia!

Na siku hizi dawa za kuongeza nguvu za kiume ziko nyingi kuna Ciallis, Levitra, Yohimbine na mengine. Hizo dawa zina side effects kama kuumwa kichwa, kuharisha, pua kuziba, macho mekundu, tumbo kuumwa na mengine mengi. Pamoja na side effects bado zina soko kubwa. Na zikipigwa marufuku nina amini kuwa watu watatajirika kwa kuzifanyia magendo.

Kwa kweli wanaume wako tayari kufa kama wakishindwa kufanya tendo la ndoa. Nashindwa kuelewa sababu. Yaani tendo la ndoa ni tamu kiasi hicho au wanahofia kuwa kwa vile hawa-‘function’ tena ndo basi si wanaume? Mtu anakuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa.

Mwanaume anaambiwa anaweza kupofuka akitumia hiyo dawa lakini bado yuko tayari kuchukua risk. Halafu mwanaume akiitwa ‘hanithi’ yuko tayari kupigana au kuua. Sijui bila kusimamisha anajiona si mtu tena…sielewi kabisa! Nikawa najadiili na marafiki zangu juzi na tulikubaliana kuwa wanaume wako tayari kuchukua ‘risks’ kuliko wanawake.

Yaani mwanaume anaweza kufanya tendo la ndoa hata akijua kuwa kuna hatari ya mwenzake kuwa na ugonjwa wa zinaa na ataambukizwa. Bongo, walikuwa wanasema eti, ‘Ajali Kazini’! Hiyo ajali inaweza kukuua! Sijui hiyo ume ikisimama ndo basi tena, akili zote zinahamia hapo.

Nauliza tena, tendo la ndoa ni tamu kiasi kwamba mko tayari kuhatarisha maisha yenu?

Kukosa nguvu za kiume zi mwisho wa dunia jamani. Bado tunawahitaji!Lakini nikirudi kwa marehemu jirani yangu, uwongo mbaya, alikuwa anatabasamu ndani ya jeneza lake!

NB:
Nyie wanaume mnaotaka kutumia hizo dawa kawaone daktari wenu kabla ya kuanza kuzitumia.


Kutoka: Chemi Che-Mponda Blog

1 comment:

MOSONGA RAPHAEL said...

Hongera kwa Chemi, hii stori inasikitisha ila wakati mwingine nimecheka sana!!!!