Wednesday 14 November 2007

Vijana Chipukizi ...!

Nakumbuka zile nyimbo nilizoimba enzi za udogo wangu Shule ya Msingi na nilipokuwa ktk Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa Sheria (baada ya kidato cha Sita)!

Shule ya Msingi Baranga mwaka 1978/79 kulikuwa na gwaride la vijana wadogo toka shule mbalimbali Baranga, Kongoto, Nyambili, Sirori Simba, Wegero n.k.
Mwalimu Mgongo toka Kongoto ndie aliyeendesha mafunzo. Mara ya kwanza yalianzia Baranga halafu tukaenda Kongoto.

Wimbo maarufu sana ninaoukumbuka ni huu:
'Vijana chipukizi, kutembea kwao kuringa kwao ni sawa-sawa ...' (mara 2)
Chorus:
'Kutembea kwao'
(kiitikio) 'Ni sawa-sawa'
'Kuringa kwao'
(kiitikio) 'Ni sawa-sawa'
'vijana chipukizi, kutembea kwao kuringa kwao ni sawa-sawa' (mara 2)

Darasani Napo tuliimba nyimbo:
Mwalimu Telesphory Paschal alikuwa anatuimbisha sana. Baadhi ya nyimbo hizo;
'row row your boat; row row your boat!' (mara 2)
'gently down the stream' (mara 2)
'merrily merrily merrily life is bad a dream!' (mara 2)

'home again, (home again)
'when shall I see my home again,
when shall I see my brothers and sisters?
Never forget my home'

'jembe ni kitu bora kwa watu wote,
jembe ni kitu bora kwa wakulima, ...'

mchaka-mchaka;
'kambonaa kakimbia azimio (azimio la arusha)'

'banda wa malawi (banda wa malawi),
katuvalia ngozi ya simba, hatujali eee hatujali.
banda wa malawi (banda wa malawi),
katuvalia ngozi ya chui, hatujali ee hatujali!'

Sijui mwanangu ataimba nyimbo kama hizi shuleni au zilishapitwa na wakati!

No comments: