Tuesday 16 October 2007

Yanga tujitegemee!

Klabu ya Yanga inatakiwa kuanzisha vitega uchumi vya uhakika na kuacha kutegemea hela toka mifuko ya wasamaria wema kila siku!
Yanga ina jengo kubwa na uwanja wake wa Kaunda.
1. Nashauri jengo likarabatiwe na nafasi ikiruhusu liongezwe (extension) na kukodisha baadhi ya nafasi kama ofisi na migahawa. Pia ukumbi nao unaweza kutumika kukodisha kwa shuguli za mikutano au tafrija mbalimbali.
2. Uwanja wa Kaunda ukarabatiwe na kuimarishwa ili utumike kibiashara zaidi kwa mechi za kirafiki au mashindano madogo madogo, ligi za madaraja ya chini au matamasha/sherehe za watu binafsi.
3. Timu inaweza kukopa benki na kupata hela za kuiendeleza kibiashara na kisayansi. Kuna wataalamu wengi ambao ni wapenzi au wanachama wa Yanga wanaweza kusaidia maendeleo ya timu.
4. timu iwe kampuni (plc) na watu hasa wanachama wanunue hisa ili kuongeza mtaji ktk mfuko wa timu.

Haya yote yanahitaji nidhamu ktk uongozi na utawala mzuri wa timu na fedha!

Kwanini Yanga inahangaika hivi miaka yote na wakati ina msingi mzuri wa kiuchumi -jengo na uwanja. Pia kuna wataalamu wa mambo ya fedha na uhandisi ambao wako tayari kutumia taaluma yao nyumbani (Yanga).
Kwanini tunaumiza vichwa kutafuta wahisani waisaidie Yanga 100% kifedha, badala ya kuumiza hivyo vichwa nini kifanyike ili timu ijitegemee -iondokane na maisha tegemezi?

Natoa wito mapinduzi ya kiuchumi, kimaendeleo yafanyike ili Yanga iwe timu kubwa Afrika kwani historia ya timu inaonyesha kuwa Yanga ikiamua MAMBO MAKUBWA yatafayika!

Hebu Yanga tuamke.

No comments: