Tuesday 2 October 2007

Dada Chemi na 'Miss Bantu Halisi!'

Marudio - Wapenzi wa Matako Makubwa (From my 12/2005 Blog):

Wapenzi wasomaji, leo nimeamua kuzungumzia suala ya matako makubwa. Tafadhali msione kama ni matusi lakini hapa USA ni issue kubwa, maana watu wanayachukia! Nimeona nizungumzie suala ya matako makubwa kwa vile jana kazini, mzungu aliyekondeana mno kasema ni mnene na akila keki eti yote itaenda matakoni. Nilishangaa na kusikitika sana.

Uzuri kwa wazungu ni kuwa na matako fleti kama vile yamepigwa pasi. Sijui kwa nini. Mtu anashepu ya mbao, mwanamke hana hips kakaa kama dume vile eti ndo uzuri. Kumbe ni kwa sababu hao models na wacheza sinema wako hivyo!Basi wasichana na akina mama wanajinyima chakula kusudi wakonde na eti wapendeze. Ndo maana magonjwa kama Bulimia na Anorexia zimeshamiri hapa.

Lakini ukitazama sinema za miaka ya nyuma kama za 1930's na 1940's, wanawake walikuwa na shepu na walikuwa wamejaa na hata wanaume wa kizungu walikuwa wanasifia. Mpaka 1950's kulikuwa na mcheza sinema Marilyn Monroe, alikuwa na zinga la figure 8, na wanaume wote walikuwa wanampapatikia. Ama kweli mambo yanabadilika. Hivi sasa wanasema eti walikuwa ni obese yaani wanene! Mbona mimi naona matako fleti kama chapati ni mabaya na hayapendezi? Au ni kwa sababu nimekulia Africa?

Brothas (waMarekani Weusi) wanapenda mwanamke awe na matako ya maana! Akipita mwanamke mwenye mbarikio utasikia brothas wakisifia, "umm, umm umm!"

Kuna siku nilisikia wanaume wa kizungu wakijadili sababu ya wanaume weusi kupenda matako makubwa, walisema ni "cultural thing". Kwa kweli ni culture yaani utamaduni wa mwafrikai! Kama umekulia katika mazingara ya kupenda kitu utakipenda. Na ndo maana kuna weusi USA wanataka kuwa na shepu iliyokondeana kama mzungu kumbe haiko katika 'genes' zake. Wajitahidi kupunguza mzigo lakini wapi, iko pale pale.

Sisi wanawake wenye asili ya Afrika tumebarikiwa huko nyuma. Yaani boxi, siha, wowowo, booty, na nasikia waGhana wanaita yokohama, matako makubwa yana majina mengi. Waafrika tunaona kama ni urembo, lakini wazungu na waliokulia uzunguni wanaona kinyaa. Wanasema eti ni dalili ya ulafi na uvivu! Lakini kama ni dalili ya ulafi mbona hata mwanamke mwembamba mwafrika anaweza kuwa na kamzigo huko nyuma?

Ubaya mwenye matako makubwa anaweza kubaguliwa kwa vile bosi anaweza kuona kuwa ni 'ugly' (mbaya) na mwenye nacho anachafua mazingira ya ofisi. Kweli kabisa! Hayo matako makubwa ni 'genes' za sisi waafrika. Lakini ajabu kuna siku nilisikia wazungu wakisema eti waafrika tuna matako makubwa kwa sababu ya utumwa. Eti mabibi zetu walinyimwa chakula hivyo matako ndo ilikuwa 'godown' ya mafuta ya akiba. Nadhani ni uzushi kama ile ya ngamia kuweka maji kwenye nundu zake!

Mimi mara nyingi nimeambiwa nina matako makubwa, niyapunguze kwa kwenda gym kufanya mazoezi. Hayo mazoezi haisadii kitu ni makubwa vile vile! Lakini msione kama naona haya, wala! Mtu akiniambia nina matako makubwa namwambia mbona kama ni madogo, na ningependa yawe makubwa zaidi! Wanabakia kushangaa hasa nikiwaambia kuwa Afrika, matako makubwa ni uzuri.Na amini usiamini kuna opresheni ya kuyapunguza inaitwa Liposuction.

Wanawake wengi weusi na wazungu wamefanya hiyo liposuction ya matako, akiwemo mwimbaji Janet Jackson. Ubaya, ni kuwa ukishafanya hiyo liposuction, mafuta yataenda kwingine mwilini, hivyo utakuwa na shepu ya ajabu!Sisi waafrika tunapenda kuringia huo mbarikio wa matako makubwa. Nilipokuwa nacheza ngoma shuleni na jeshini, tulikuwa tunatia nguo ndani ya bukta kusudi tuonekana na matako makubwa kweli kweli! Lakini, mara nyingi mitaani hapa USA, nimesikia akina dada wakifokewa, "You got a big a-s!"

Kuna siku nilikuwa kwenye kituo cha Subway hapa Boston, kapita mama fualni Mganda, aisei alikuwa amejaliwa kweli huko nyuma, mpaka nikaona wivu. Basi ungeona wazungu walivyokuwa wanamtazama kwa mshangao ungecheka. Ila nilishuhudia baba fulani Mmarekani Mweusi akimtazama kwa furaha na kawa kama vile anamezea mate.

Nampenda sana mecheza sinema, Whoopi Goldberg. Nilikuwa nasoma jinsi akienda kwenye audition au akiwa kwenye movie shoot, wazungu wanamwambia kuwa ana matako makubwa au avae nguo ya kuzificha. Yeye alichoka, na mwishowe kusema, " Mimi ni mwanamke mweusi, nina matako makubwa niache kama nilivyo!" Wanawake weusi wote tungedai heshima ya matako kama Whoopi nadhani wazungu wangeheshimu matako yetu makubwa.

Tatizo linigine la kuwa na matako makubwa USA ni kupata nguo. Ukienda kununua sketi au gauni uanweza kukuta mbele refu nyuma umepanda. Au unavaa hiyo nguo lakini kwenye hips na matako haipiti! Hii ni kwa sababu nguo imeshonwa kwa ajili ya wazungu wenye matako fleti. Na kupata Jeans inayofiti ni vigumu. Mtu ambaye atatengeneza nguo 'molded for the black woman' atapata wateja kweli kweli, maana tunalilia nguo kama hizo.

Pamoja na yote haya sasa wazungu wameibuka na staili ya kuwa ka ka-butt. Yaani jeans inakuwa na pedi ndani kusudi mtu aonekana ana matako. Loh! Watu hawaridhiki! Sijui tuseme asante J-Lo (mwimbaji Jennfier Lopez) au nini. Kwanza walikuwa wanamcheka J-Lo na matako yake makubwa lakini naona watu wanaanza kuyapenda. Mpaka kuna opresheni sasa ya kuongeza matako.

Wacha wafanye haitapendeza kama matako natural tulyiozaliwa nayo waafrika.

Matako Makubwa Oyee!


source: Chemi's Blog

No comments: