Saturday 4 October 2008

Nani asiyejua ID ya mgonjwa ni siri?

Mgonjwa yeyote huwa analindwa juu ya haki yake ya usiri (privacy) kuhusiana na ugonjwa wake. Madaktari au manesi huwa hawaruhusiwi kisheria kutaja hadharani jina la mgonjwa na tiba au ugonjwa anaotibiwa hospitalini. (Labda mgonjwa mwenyewe aamue kutangaza au kusema hadharani -hiyo ni hiyari yake!). Ila leo nimeshangaa kusoma haya ktk gazeti la Nipashe (on-line)!!!
.......................
.......................

Mgonjwa wa akili aliyejeruhiwa atoka ICU
Hali ya mgonjwa wa akili, Athuman Abdallah, ambaye alivamiwa na kuumizwa na mwezake na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa kichwa, inaendelea vizuri na amerudishwa wodi ya wagonjwa wa akili. Awali, Abdallah alilazwa chumba cha wagonjwa wenye Kuhitaji uangalizi maalum (ICU), akipatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa na David Dege ambaye ni mgonjwa wa akili.

Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Mifupa (Moi), Almas Jumaa, alisema hali ya Abdallah imeimarika kiasi cha kurejeshwa wodini kuendelea na matibabu ya akili. Jumaa alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuonekana anaweza kuchanganyika na wenzake kama ilivyokuwa awali kabla ya kushambuliwa. Aliongeza kuwa anachofanyiwa mgonjwa huyo kwa sasa ni kuletwa kliniki kwa ajili ya matibabu ya kawaida kujua jinsi anavyoendelea.

(SOURCE: Nipashe, 2008-10-04 11:29:56 Na Godfrey Monyo)

1 comment:

MOSONGA RAPHAEL said...

Mgonjwa wa akili aliyejeruhiwa atoka ICU

2008-10-04 11:29:56
Na Godfrey Monyo


Hali ya mgonjwa wa akili, Athuman Abdallah, ambaye alivamiwa na kuumizwa na mwezake na kulazimika kufanyiwa upasuaji wa kichwa, inaendelea vizuri na amerudishwa wodi ya wagonjwa wa akili.

Awali, Abdallah alilazwa chumba cha wagonjwa wenye Kuhitaji uangalizi maalum (ICU), akipatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa na David Dege ambaye ni mgonjwa wa akili.

Katika shambulio hilo, Denge inadaiwa kutumia chuma kushambulia wenzake na kusababisha vifo vya watu wawili.

Kufuatia tukio hilo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, aliunda tume iliyobaini kuwepo uzembe katika kuhudumia wagonjwa hao.

Katika tukio hilo, mgonjwa mwingine Hamis Gangira naye alijeruhiwa.

Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Mifupa (Moi), Almas Jumaa, alisema hali ya Abdallah imeimarika kiasi cha kurejeshwa wodini kuendelea na matibabu ya akili.

Jumaa alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuonekana anaweza kuchanganyika na wenzake kama ilivyokuwa awali kabla ya kushambuliwa.

Aliongeza kuwa anachofanyiwa mgonjwa huyo kwa sasa ni kuletwa kliniki kwa ajili ya matibabu ya kawaida kujua jinsi anavyoendelea.

Waliokufa katika shambulio hilo ni Paul Maganga na Abdallah Abeid.

SOURCE: Nipashe