Friday 31 October 2008

Tulikotoka: RTD

Nimeambiwa kuwa siku hizi RTD inaitwa TBC 1. Zamani nilipokuwa mdogo nilipenda sana Vipindi vya Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) (miaka ya 1980).

Kwanza ni anuani yao:
Pugu Road (Nyerere RD siku hizi), SLP (POBox) 9191 Dar es Salaam.

Vipindi:
Taarifa ya Habari; ngoma za Moris Nyunyusa zilianza kutukaribisha na kutusogeza karibu na redio, kisha ti, ti, ti, ... (mara 6) Kisha; ...
'Hivi sasa ni saa ... kamili', (Mwanadada alisikika akisema)
(kisha akafuatia msoma habari)
Na hii ni taarifa ya habari kutoka Redio Tanzania Dar es Salaam,
Msomaji ni Charles Hilary, au Betty Mkwasa n.k
kwanza ni mkhutasari wake ....
habari kamili. Mwanza. Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais ....
baada ya dakika tano ...
'mnaendelea kusikiliza taarifa ya habari kutoka redio tanzania dar es salaam'
Tokyo ......
baada ya dk 9 hivi,
'kwa kumaliza taarifa ya habari, sikilizeni tena muhtasari wale'
waziri mkuu na .....
baada ya dk 10,
na huo ndio mwisho wa taarifa ya habari kutoka redio tanzania daresalaam.

Tunawaletea mazumzo baada ya habari (saa 2 usiku, saa 10 alasiri au saa 1 asubuhi).
baada ya dk 5
mazungumzo baada ya habari yamewajia kutoka redio tanzania daresalaam.

au badala ya mazungumzo baada ya habari kuna matangazo ya vifo.

Enzi hizo hakuna redio za watu binafsi. RTD ilikuwa na idhaa 2, ya Taifa (nchi nzima) na ya biashara ikisikika zaidi Dar na maeneo jirani au maeneo ya mijini zaidi.

Vipindi zaidi nilivyovipenda
Misakato
Michezo (michezooo) saa 2 kasorobo usiku
Mama na Mwana (hasa mtangazaji wake mama Debora Mwenda)
Kumekucha (miziki)
Asubuhi Njema (baadae kikaitwa Jambooo) (miziki ya dansi)
Mchana Mwema (miziki ya dansi)
Ombi Lako (baadae kikaitwa 'chaguo lako' (miziki)
Hotuba za Baba wa Taifa saa 2:15 - 2:30 usiku (Jumatatu - Ijumaa)
Mahoka (vichekesho)

No comments: