Thursday, 9 October 2008

Ikulu TZ yatumia anuani ya 'yahuu'!

Ni aibu ilioje kwa Ikulu ya Taifa letu kutumia e-mail address 'za mitaani' ktk mawasiliano na wananchi wake! Huu ni ukata au kutokuwajibika?

Kwa vile Ikulu ina tovuti yake (ikulu.go.tz) basi ni vema wangetumia e-mail hii (mfano): mawasiliano@ikulu.go.tz.

Pia nashangaa kuwa kwa wanaotumia lugha ya kiingereza kupewa anuani rasmi ya Ikulu na wale wanaotumia lugha ya Taifa kupewa anuani ya 'mitaani'! Kwa namna moja au nyingine hii aina mojawapo ya ubaguzi!
....................................................
....................................................
Barua kutoka Ikulu kwa wananchi ni hii hapa (nimeipata lukwangule.blogspot.com).

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nchi za Afrika zimeonywa kuwa macho na uwezekano wa kugeuzwa soko kubwa la madawa ya kulevya kutoka Marekani Kusini, hasa baada ya Marekani kuwa imedhibiti soko lake.

Onyo hilo limetolewa leo (Jumanne, Oktoba 7, 2008) na Balozi mpya wa Colombia katika Tanzania, Mama Maria Victoria Suarez wakati alipokutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu, Dar es Salaam.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
07 Oktoba, 2008
..................

No comments: