Monday, 13 October 2008

Stars bado ina pointi 3 tuu?! No Noo Nooo!

Gazeti la Majira la leo limeniacha hoi. Linadai eti timu ya Taifa (Stars) imemaliza michuano ya kwania kombe la dunia na mataifa ya Afika ikiwa na pointi tatu tu pamoja na ushindi wa jana!
Mimi siamini haya ya Majira kwani kumbukumbu zangu (ingawa sifuatilii sana michuano hii) zinaniambia kuwa Stars ilitoka sare na Mauritius 1-1 na pia ikatoka suluhu na Cameroon 0-0. Halafu iliifunga Mauritius 4-1 na jana ikaifunga cape Verde 3-1. Ilifungwa mechi mbili na Cameroon na Carpe Verde. Kwa hesabu za haraka haraka Stars ina pointi 8.
...................................................
Soma sehemu hii kutoka gazeti Majira 13/10/2008.
'Stars juzi ikicheza soka la uhakika, iliifunga Kepuvede mabao 3-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi la Kwanza katika harakati za kufuzu fainali hizo, ambapo licha ya ushindi huo haijafuzu kwani imemaliza ikiwa na tatu na pointi nane nyuma ya Kepuvede yenye pointi tisa na vinara Kameruni wenye pointi 16'.

No comments: