Wednesday 11 July 2007

Yanga, Kocha mpya na nilichokisema!

Micho ruksa kuondoka Yanga
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa ruksa kwa kocha wao Mserbia, Milutin Sredojevic `Micho` kuondoka endapo hatarejea nchini baada ya kuomba kwenda kwao Serbia kutibiwa. Akizungumza jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo Iman Madega alisema kuwa safari ya kocha huyo inabaraka zote za uongozi, ambapo yeye mwenyewe aliahidi kurudi nchini kuendelea na kazi yake, lakini endapo hatarejea, timu yao haitatetereka. Madega, alisema kuwa wao hawawezi kumzuia Micho kujiamualia mambo yake, ambapo alisema kuwa hata kama hatarudi nchini kama alivyoahidi Yanga itaendelea kuwepo na itashiriki katika michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo. ``Tunataarifa na safari yake na alituaga muda mrefu tu, ametuahidi atarudi nchini kuendelea na kazi yake, lakini hata kama atabadili maamuzi sisi hatuwezi kumuzia kwani hayo yatakuwa tayari ni maamuzi yake ila Yanga itaendelea kuwepo,`` alisema Madega. Madega, aliongeza kuwa uongozi wake unauhakika mkubwa kuwa Micho hajaikimbia timu hiyo, na alisema kuwa mara baada ya kukamilisha matibabu yake atarejea nchini kuendelea na kazi yake. Alisema kuwa Micho, amekwenda kwao kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi hasa baada ya kupoteza kiasi cha kilo saba za uzito wa mwili wake kutokana na kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa kuharisha na kutapika. Ni kocha wa kimataifa na mwenye sifa zote za kocha wa kimataifa hivyo anastahili kupata matibabu mazuri zaidi na ndio maana aliamua kwenda kwao na kwa kuwa hiki ni kipindi cha mapumziko hatukuona sababu ya kumkatalia,`` aliongeza Madega. Aidha, Micho mwenyewe muda mfupi kabla ya kuondoka alilithibitishia Nipashe kuwa anakwenda kwao kupata matibabu zaidi, na aliahidi kurudi nchini kuendelea na kazi yake. Micho, ameondoka siku mbili baada ya timu yake kuvuliwa ubingwa wa Bara baada ya kufungwa kwa penati 4-3 na watani wao wa jadi Simba, baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 hadi dakika 120 zinamalizika.
SOURCE: Nipashe, by Jimmy Charles 11/7/2007.

Nilichosema mwaka jana!
(Natoa) Hongera kwa Yanga kutwaa ubingwa 2006. Nawatakia kila la heri mwakani Champions League ya CAF. Yanga hawana haja kuleta kocha mpya kwa sasa, waliopo wanafaa. Wanachotakiwa kufanya ni kukarabati uwanja wa Kaunda ili utumike ipasavyo (kibiashara) kama kitega uchumi. Pia Yanga wanatakiwa waweke au waongeze facilities za kisasa za mazoezi kwa wachezaji na huduma nyingine (e.g. hospitality) klabuni.
(Hii ni sehemu tu ya nilichosema mwaka jana hata kabla kocha Chamangwana hajavuliwa madaraka!)

No comments: