Friday 22 June 2007

Shirikisho la afrika Mashariki*

Nimesoma makala yako kuhusu viongozi wetu na shirikisho.
Ninakubaliana nawe hasa uchambuzi wa kisiasa na kiuchumi ulioufanya. (Naona kama ulisahau kuongelea Rwanda na Burundi ambazo zimeongezwa ktk jumuiya ya A. Mashariki)
Uzoefu wako hasa ktk jumuiya ya zamani ni wa kipekee kwa vile kizazi cha viongozi/wabunge wa sasa wamesahau mabaya yaliyosababisha kuvunjikka jumuiya na jinsi Kenya ilivyotudhulumu.
Pamoja na makundi yote uliyobainisha kuwa yashirikishwe kikamilifu, mimi napenda kuongezea kundi ambalo ni muhimu kisiasa na ki-ushawishi. Kundi hili ni Vyama Vya Siasa. Unaonaje viongozi wa vyama hivi nao wakipiga kampeni kuwaelimisha wananchi juu ya madhara ya shirikisho kwa nchi yetu?
Nimejaribu kuongea na watu mbalimbali na nimegundua kundi la watu wanaotaka shirikisho ni wanasiasa ambao wana nafasi ya kupata ulaji/uongozi ktk shirikisho hasa marais wetu mfano hao waliobadilisha katiba zao ili wawepo madarakani ktk kipindi cha kuanzisha shirikisho!!
Watu wengine wanaotaka shirikisho ni wafanyabiashara (wachache) wakubwa ambao watanufaika na kutangaza/kusambaza biashara zao ktk nchi hizo zote.
Ninaamini wananchi walio wengi Tanzania hawatanufaika.
Ningependa kuona unaazishwa mtandao wale wananchi wanaopinga kuanzishwa kwa shirikisho ili wawe msitari wa mbele kuwaelemisha wananchi na kuwashinikiza viongozi wetu wawasikilize wananchi. sidhani kama ni vibaya huo mtandao kuwepo!
Tunaomba pia wabunge wetu watuwakilishe kikamilifu ktk hili.
Kuna mambo mengi ambayo tungependa serikali yetu iyashughulikie badala ya kupoteza nguvu na muda kwa hili la shirikisho.


*Barua hii niliiandika tarehe 27/12/2006 kama maoni yangu binafsi.

No comments: