Tuesday 26 June 2007

Mhe Mzindakaya; habari zaidi za nyumbani leo.

MBUNGE wa Kwela (CCM), Dk. Chrisant Mzindakaya, amekana kuwa sehemu ya ubadhirifu ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama ilivyodaiwa na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa (CHADEMA).
Akitoa maelezo bungeni juzi, baada ya Dk. Slaa kueleza hayo, Mzindakaya alikiri kukopa katika benki ya biashara kwa dhamana ya serikali na kwamba hajakopaau kudhaminiwa na BoT.Alisema mwaka 2004, serikali ilianzisha sera yakuwawezesha Watanzania ambao miradi yao inaonekana ina manufaa kwa uchumi wa nchi.
"Ingawa nia ya serikali wakati ule ilikuwa ni kuitumia Benki ya Rasilimali nchini (TIB) kwa miradi ya kilimo na ile ya ufugaji, benki hiyo ilikuwa bado haijajiandaa kikamilifu. Kwa hiyo serikali ilitoa mwongozo kuwa, kwa wakati ule wenye miradi waende katika benki watakazokuwa wamechagua na benki hizo kuwakubalia."... benki husika ndiyo zitaandika barua serikalini na kwa Benki Kuu na badala ya serikali kutoa udhamini kwa benki iliyotoa mkopo, serikali ilitoa dhamana kwaBenki Kuu," alisema Dk. Mzindakaya.Alisema mdhamini wa mkopo wake si BoT, ni serikali kupitia Wizara ya Fedha na kuongeza: "Mkopo wa Standard Chartered Bank si wa muda mrefu, mara nyingiwanatoa mkopo wa muda mfupi usiozidi miaka mitano".
Dk. Mzindakaya alisema mradi alioombea mkopo ni wa ufugaji wa ng'ombe wa nyama, ujenzi wa machinjio na kiwanda cha kisasa, ambao ulipaji wake hauwezi kuwa wa muda mfupi."Kwa kuwa Standard Chartered waliridhika kwamba mradi huu ni mzuri walikubali kutoa mkopo huo, na kwa kuwa muda wao ni miaka mitano, baada ya mradi wenyewe kuanza kutekelezwa... walitoa pendekezo kwa serikalikwamba ni mzuri, lakini mkopaji hawezi kulipa kwa miaka mitano."Walipendekeza serikali ipeleke katika benki nyingine Mambayo muda wake utakuwa mrefu kwa mkopaji. Baada ya hayo benki niliyokopa ambayo sina haja ya kutoa maelezo mengi, ilipopeleka mapendekezo yake, serikaliilikubali kwa kuzingatia umuhimu na faidia ya mradi huo."Baada ya kukubali, serikali yenyewe ndiyo iliagiza BoT kwamba mimi sasa nihamie TIB. Kwa hiyo mkopo niliokopa mimi na dhamana ni ya Serikali Kuu na si ya BoT," alisema Dk. Mzindakaya.Alisema BoT haiwezi kumkopesha kwa sababu haiwezi kukopesha mtu, haina hela ya kukopesha. Aliongeza: "Fedha nilizokopeshwa, mdhamini wake narudia ilikuwa Serikali Kuu na fedha ambazo ilionekana lazima nihamie TIB, serikali ndiyo imelipa katika benki niliyokopa na siyo Benki Kuu kama inavyoelezwahapa."Mzindakaya ambaye ni mbunge wa Kwera-CCM, alisema hawezi kueleza kuhusu kiwango cha deni la kampuni yake na kuwa deni ni siri kati yake na benki,hivyo takwimu zilizotolewa hawezi kizithibitisha kwa sababu ni siri ya mkopaji na mkopeshaji.Dk. Mzindakaya alisema kiwanda kilichojengwa kitatoa ajira kwa wafanyakazi 180 na wale wasiokuwa wa moja kwa moja watakuwa 2,300, hivyo kuwa na manufaa kwa Watanzania.
"Ninaweza sasa nikatambua kwamba mtu mweusi kufanya maendeleo ya aina hii tuliyofanya ni dhambi kwa sababu hakuna atakaye- appreciate jambo kama hilo, na leo (juzi) maelezo haya ni ushahidi. Si kweli kwamba kampuni yangu imeomba mkopo mwingine wa mabilioni kutoka Benki Kuu."Sikujua kama lengo la maelezo ya Dk. Slaa ni gavana kwa jina la Ballal. Nilisema baadhi ya mambo mazuri, ambayo BoT imeyafanya katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
"Sijatetea maovu yoyote ambayo yanamlenga gavana kwa sababu mimi sikujua hayo.
Nilisifu serikali kwamba imekubali na itafanya ukaguzi wa yanayozungumzwa kuhusu Benki Kuu. Nimekuwa mtetezi na nimeendelea kuwamtetezi wa wananchi kupitia sera za chama changu," alisema.Alisema katika kipindi cha miaka 40 alichofanya kazi hiyo, hajawahi kuhusishwa na kashfa yoyote katika maisha yake na kuongeza kuwa kuwa: "Nimekopa katika benki sikuiba, wala siku- Collude na Benki Kuu."
Dk. Slaa akiwasilisha hotuba ya kambi ya upinzani kuhusu makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2007/08, alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 49 (7), ambacho kinamzuiambunge kuzungumzia jambo ambalo ana maslahi nalo kifedha, isipokuwa baada ya kutaja jinsi anavyohusika na kiwango cha maslahi hayo, Dk. Mzindakaya hakutaja maslahi yake kuhusu BoT.
Alisema utafiti wao umeonyesha kuwa mwaka 2004, Dk. Mzindakaya alichukua mkopo kwa shughuli za kampuni yake binafsi ya SAAFI wa sh. bilioni 6.217 kutoka benki ya Standard Chartered.Dk. Slaa alisema BoT ilidhamini mkopo huo na kwamba mwaka huu, benki hiyo kutokana na mdhamana tayari imelipa sh. bilioni 8.1 kwa niaba ya Dk. Mzindakaya na fedha hizo na riba zinakisiwa kufikia sh. bilioni 9.7, deni ambalo limehamishiwa TIB, ambako anatakiwa kulipa deni la BoT."Hivi sasa ameomba adhaminiwe na BoT mkopo mwingine wa sh. bilioni mbili. Mkopo huo uko katika hatua ya kujadiliwa na BoT," alisema Dk. Slaa.
Spika wa Bunge, Samuel Sitta alihitimisha hoja hiyo akisema: "Naridhika kwamba kwa kuwa mkopo ulikuwa wa kibiashara, alikuwa hana haja ya ku-declare conflict of interest yoyote kwa sababu hata guarantee yenyewe kumbe ni ya serikali. Kwa hiyo hakuathiri Kanuni ya 49 (7)."


JK: Sheria ya dawa za kulevya ifanyiwe marekebisho haraka 'Mateja' sasa kupewa matibabu kwa nguvu

RAIS Jakaya Kikwete amesema sheria inayotoa adhabu ndogo kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya itaangaliwa upya na kutupilia mbali hoja za wanaodai kutetea haki za binadamu.Alisema watuhumiwa hao wamekuwa wakiharibu watoto, lakini wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria hupewa adhabu ndogo kuliko makosa yanayofanywa kwa kigezo cha kuheshimu haki za binadamu.Akizungumza kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga jana, Rais Kikwete alisema inashangaza kuona mtu anakamatwa na dawa za kulevya zenye thamani ya milioni 30, lakini anapewa adhabu ya kulipa sh. milioni moja."Naomba niseme sifurahishwi sana na sheria kwamba mtu anakamatwa na dawa za sh. milioni 30, lakini anatozwa faini ya sh. milioni moja. Hii inashangaza sana kwa nini huyu mtu asifungwe jela miaka ya kutosha ili akitoka awe amezeeka na hiyo itatusaidia kuinusuru jamii yetu," alisema.Rais Kikwete alisema kama mtu ameweza kununua dawa zenye thamani ya mamilioni anapaswa kuogopwa na kupewa adhabu kubwa na kwamba akiachiwa ataendelea kufanya biashara hiyo na kuiharibu jamii ya Watanzania.

Watendaji walaumiwakukwamisha maendeleo

BAADHI ya wabunge wamewashutumu watendaji wa serikali kwa kukwamisha kasi ya maendeleo ya wananchi, kwa kutumia fedha kinyume cha malengo yaliyokusudiwa.Wabunge Mudhihir Mudhihir (Mchinga-CCM), Diana Chilolo (Viti Maalum-CCM), Vedastusi Manyinyi (MusomaMjini-CCM) na Omar Kwaangw' (Babati Mjini-CCM), kwa nyakati tofauti walilalamikia baadhi ya watendaji wanaokwamisha maendeleo.Mudhihir alimlalamikia katibu tawala wa mkoa kwa kukwamisha mradi wa ujenzi wa hospitali, ambao uliwahi kutengewa sh. milioni 300, zilizohamishiwa kwenyemradi mwingine, wakiambiwa kuwa wao ni 'sikio katika uso'.Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa wababe na wanakiuka Katiba. Alisema hospitali hiyo ni muhimu kama ilivyo ya Tumbi, Kibaha, ambayo itasaidia hatamajeruhi.Akizungumzia kuhusu umeme kutoka Mnazi Bay, Mudhihir alisema sh. milioni 320 zilitengwa kwa ajili ya kazi hiyo, lakini ofisa mmoja wa Wizara ya Fedhaamekwamisha kazi hiyo.Diana kwa upande wake, alisema mwaka 2005 walitengewa sh. milioni 200 na mwaka 2006 walipewa sh. milioni 165 kwa ajili ya ununuzi wa gari la zimamoto, lakini sh.milioni 165 zilitumiwa kwa shughuli tofauti.Alisema Singida imekuwa ikikabiliwa na majanga ya moto kama ilivyotokea hivi karibuni kwa basi la Mohamed Trans kuungua, lakini walishindwa kuwasaidia kutokana na kutokuwepo kwa gari la zimamoto. Alitaja majengo mengine yaliyowahi kuungua kuwa ofisi ya CCM, stendi ya mabasi na nyumba ya mfanyabiashara."Tutaendelea kuipaka matope serikali hadi lini. Wanajua taratibu za fedha, tuwatazame kwa macho mawili watu wa aina hii. sh. milioni 200 zilizobakituongezewe tupate gari la zimamoto," alisema. Manyinyi alisema wako baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakisababisha kero kwa wananchi pasipo sababu, moja kati ya hizo ikiwa magari kukamatwa kwa kutokufungwa vidhibiti mwendo, ambavyo havipo.Kwa upande wake, Kwaangw' alisema ubadhirifu uko kwenye manunuzi ya vifaa, huduma na ujenzi, alishauri Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi (PPRA) ifanye kazi hiyo na si Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikalipekee. Katika hatua nyingine, wabunge wameishauri serikali kuwa posho ya madiwani ya sh. 60,000 kwa mwezi itolewe kwa halmashauri zote na si kwa kulingana na uwezo wake.Wabunge hao Diana, Jenista Mhagama (Peramiho- CCM), Estherina Kilasi (Mbarali- CCM) na Manyinyi walisema hayo walipokuwa wakichangia hotuba ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi yake na ofisi ya bunge kwa mwaka 2007/08.
Lowassa katika hotuba yake juzi alisema serikali imekubali kuongeza posho za madiwani kutoka sh. 30,000 hadi sh. 60,000 kwa mwezi, kulingana na uwezo wa halmashauri. Alisema kazi ya kutathmini halmashauri zisizo na uwezo inaendelea kufanyika. Diana aliishauri serikali kuongeza kiasi hicho kifikie sh. 100,000 na kwamba posho hizo zilipwe na serikali kuu.Katika hatua nyingine, Estherina aliishauri serikali nusu ya fedha kwa ajili ya wajasiriamali zitolewe kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo(SIDO) kutokana na benki kushindwa kuwapatia mikopowakulima.Baadhi ya wachangiaji kwa nyakati tofauti, waliwataka mawaziri kwenda majimboni kujibu kero za wananchi, kwa kuwa wao wamekosa majibu.

No comments: