Monday 25 June 2007

Maoni: Yanga Tuamke Kumekucha!*

(Natoa) Hongera kwa Yanga kutwaa ubingwa 2006. Nawatakia kila la heri mwakani Champions League ya CAF.
Yanga hawana haja kuleta kocha mpya kwa sasa, waliopo wanafaa.
Wanachotakiwa kufanya ni kukarabati uwanja wa Kaunda ili utumike itasavyo (kibiashara) kama kitega uchumi. Pia Yanga wanatakiwa waweke au waongeze facilities za kisasa za mazoezi kwa wachezaji na huduma nyingine (e.g. hospitality) klabuni.
Long term plans:
Yanga watafute site kwa ajili ya uwanja wao kwa mechi za nyumbani wenye capacity kati ya watu 20,000 hadi 25,000 (au zaidi ya hapo). Kama kampuni, wana nafasi ya kupata mkopo kwa ajili hiyo. Faida nyingine ni kuwa uwanja utakuwa unaazimwa/unakodiwa na TFF au timu yoyote ya Tanzania kwa mechi za kimataifa na za CECAFA, CAF au FIFA na timu itapata fedha (hata za kigeni). Pia itaondokana na kuilalamikia TFF kupunjwa mapato hasa mgawanyo wa ki-asilimia wa viingilio, maana itapanga viingilio vyake na kuuza tiketi yenyewe. Kwa hiyo itadhibiti udokozi na ubadhilifu unaofanywa U/Taifa kwa sasa.
Hebu fikiria Man Utd ktk uwanja wake wenye uwezo wa watazamaji zaidi ya 76,000, wanatoa tiketi kwa timu pinzani inayokuja kucheza Old Trafford tiketi 3,000 - 6,000 tu. Hii ina maana kuwa tiketi zilizobaki 70,000 - 73,000 zinauzwa na timu yenyewe (Man Utd). Tuchukulie kwa mfano, kwa wastani, tiketi moja ni GBP 20 kwa hiyo Man Utd wanapata, angalau, GBP 1,400,000 ktk mechi moja ya nyumbani (hizo ni paundi!!!).
Nadhani Yanga nao waige hili maana ni zuri na ni endelevu. Mathalani, ktk uwanja wa viti 20,000 kwa bei ya sh.2,500 kiingilio, Yanga wanaweza kuingiza sh.50,000,000/= ktk mechi moja ya kawaida mfano dhidi ya Mtibwa au Prisons. Siku ya mechi dhidi ya Simba kwa kiingilio cha sh.4,500 itakuwa jumla sh.90,000,000/=.
Ukipata hiyo hela ya 1. viingilio, 2. ukodishaji uwanja na 3. ukiongezea hela inayoingia ktk udhamini mbali mbali na matangazo Uwanjani, timu itapata mapato makubwa na itaweza kujiendesha kibiashara zaidi badala ya kutegemea kina ''Yanga Family'' wagharamie usajili wa timu kila mwaka. Au kutegemea kina Aaron Nyanda watoe hela ya nauli/posho kwa wachezaji baada ya mazoezi; kisa, eti hakuna hela ya posho kwa wachezaji kambini!!! Hii hali inasikitisha hususan kwa timu kama Yanga, mabingwa kwa mara ya tatu chini ya Chamangwana.
Pia ikumbukwe timu inahitaji kuwa na chemichemi ya wachezaji wa siku zijazo (academy). Watoto wenye vipaji wa makundi ya kiumri kuanzia miaka 11-14, 15-17 na 18-21. Kundi la muhimu zaidi ni la miaka 16-19 maana wanakuwa wanamalizia au wamemaliza elimu ya sekondari.
Inabidi kufanyike mabadiliko ya haraka kimaendeleo ili timu isonge mbele ktk enzi hizi za kiteknolojia. Hapo tunaweza tukafanya vizuri kimataifa na hata kuuza wachezaji nje ya nchi hasa kwenda nchi za EU na timu itapata hela nyingi za kigeni kwa kuuza vipaji.

*Hii ni sehemu ya barua zangu mwaka jana (2006) kwa mashabiki wenzangu baada ya Yanga kutwaa ubingwa chini ya kocha Jack Chamangwana kutoka Malawi. Sijui kwa sasa Chamangwana yuko wapi na anafanya nini. Nampongeza sana kwa kazi yake Yanga.

No comments: